Home » »

Watu saba wakamatwa na Bunduki na Risasi 59 jijini Da res salaam.


JESHI la Polisi limefanikiwa kukamata Silaha, watuhumiwa wa uhalifu wa kutukia silaha katika oparesheni iliyoendeshwa kwa nyakati tofauti katika Jiji la Dar es Salaam.
 
Kamishna wa Polisi  Kanda Maalumu ya Jiji la Dar es Salaam(DCP), Simon Sirro alisema baadhi ya silaha hizo ni pamoja na bunduki aina ya SMG na jumla risasi 59.
 
Sirro alisema kuwa tarehe Juni 3 mwaka huu mtuhumiwa Hemed Mrisho anayejulikana kwa jina la Buda (31) mfanyabiashara, mkazi wa Tabata Kinyelezi alikutwa na bunduki hiyo iliyofutwa namba zake ikiwa na jumla ya risasi 10.
 
“Mtuhumiwa alikamatwa kutokana na taarifa  kutoka kwa msiri kuwa anajihusisha na uhalifu wa kutumia silaha na uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa alikuwa akishirikiana na wenzake ambao wanasakwa” alisema Sirro.
 
Alisema katika tukio lingine Jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata bastola moja na maganda ya risasi aina ya SMG maeneo ya Kiwalani Minazi mirefu wilaya ya Ilala.
 
Alisema kuwa bastola hiyo yenye namba 05532 ilikutwa eneo la tukio baada ya majambazi kuitelekeza mara baada ya kuzingirwa na wananchi waliotaka kuwakamata.
 
“Majambazi hao walikuwa wamefanya tukio la uporaji maeneo ya Vingunguti wakitumia pikipiki aina ya boxer na katika tukio hilo walimpiga mtoa taarifa na kitako cha bunduki waliyokuwa nayo na kumpora pikipiki na pesa taslim shilingi 300,000 lakini  hata hivyo walifanikiwa kutoroka” alisema Sirro.
 
Aliongeza kuwa katika operesheni iliyoendeshwa Mei 25 mwaka huu na idara ya Interpol jijini Dar es Salaam ya kukamata magari, madawa ya kulevya na uhalifu mwingine walifanikiwa kukamata vipande 20 vya pembe za ndovu.
 
Sirro alisema katika tukio hilo maeneo ya Kimara Suka katika ukaguzi huo alishuka kijana mmoja mwenye umri kati ya miaka 39 na 45 kwa dhumuni la kukodi pikipiki na alipowaona askari alitupa kifurushi na kukimbia.
 
Katika tukio lingine jeshi la polisi walifanikiwa kukamata kontena lenye namba 00LU2876031 likiwa na rola 15 za nyaya za umeme mali ya Tanesco pamoja na watuhumiwa saba.
 
Sirro alisema kuwa nyaya hizo zinathamani ya shilingi milioni 150 zilizoibiwa Februari 26 mwaka huu zikiwa zinasafirishwa kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini (REA).
 
“Tulipata taarifa kwa msiri kuwa kuna kontena limefichwa katika kiwanda cha kutengenezea matofali na Polisi walipofika walimpata mmiliki aliyetambulika kwa jina la Donesia Aidan (40) ambaye ni mtuhumiwa wa sita na walipopekua kontena hilo walikuta rola za nyaya zipatazo 15” alisema Sirro.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog