MAUWAJI YAENDELEA KUTIKISA TARIME

Hali ya usalama Tarime imezidi kutoweka baada ya jambazi lisilofahamika likiwa na bunduki ambayo haijafahamika aina yake kuendelea kuua watu kwa risasi hasa wa jinsi ya kiume, ambapo idadi ya waliouawa imefikia saba hadi sasa na inadaiwa huwaua watu na kupotea bila kutambuliwa.
Jambazi hilo lisilofahamika liliua watu hao usiku wa Januari 27, mwaka huu katika maeneo ya Nkende likianza na kumuua Mwendesha Bodaboda, Juma Marwa Mkazi wa Nkende mjini Tarime akiwa anaelekea nyumbani kwake ambaye alikufa akiwa hospitali akipatiwa matibabu.
Mganga wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, Marco Nega alisema tangu Januari 27 hadi sasa hospitali imeendelea kupokea watu waliouawa na majeruhi ambao wamefanyiwa uchunguzi na kugundulika wakiwa wamejeruhiwa kwa risasi katika sehemu mbalimbali za mwili na kwamba watu wapatao 7 wamekwisha kufa mpaka sasa.
“Tumepokea maiti za watu na majeruhi na tumewafanyia uchunguzi wakagundulika wana majeraha ya risasi sehemu mbalimbali za mwili, ambapo tayari watu saba wamekufa wengine wamekufa wakiwa njiani wakienda kwenye matibabu Musoma, marehemu hadi ni saba,” alisema Nega.
Waliojeruhiwa wakosa huduma ya X-ray
Watu waliojeruhiwa wameshindwa kupatiwa huduma ya X-Ray kutokana na Hospitali ya Wilaya kutokuwa na huduma hiyo kwa muda wa zaidi ya miezi 3 na kusababisha wagonjwa kusafirishwa kwenda Musoma na Mwanza kwa matibabu, ambapo Samweli Richard amekufa akiwa njiani kuelekea Musoma kwenye matibabu ikiwamo huduma hiyo ya X-ray.
Hospitali ya Wilaya yashindwa kutoa huduma
Huduma kwa wagonjwa mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya imeshindwa kuendela vilivyo baada ya kupatwa na misiba miwili ya watumishi wawili, ni baada ya waume zao kuuawa na jambazi hilo lisilofahamika.
Awali Januari 26 jambazi hilo lilimuuwa Robert Kisiri (45) mkazi wa Mugabiri ambapo Mstaafu wa JWTZ Zacharia Mwita(58) na Erick Makanya (25)wote wakazi wa Kijiji cha Mogabiri Kata ya Kitare Wilayani Tarime walikutwa wakiwa wameuawa na miili yao ikiwa na majeraha ya risasi mbavuni kushoto na mgongoni.
Pia jambazi hilo liliwajeruhi watu watano kwa risasi ambao ni Mgosi Marwa Mkazi wa Mogabiri, Joseph Richard Mkazi wa Rebu, Gastor Richard Mkazi wa Rebu, Juma Mwita Mkazi wa Mogabiri na Mkandarasi Binafsi wa ujenzi, Mwasi Yomami ambao kati ya hao wawili wamefariki wakati wakipatiwa matibabu.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Justus Kamugisha amesema wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuwa mhusika wa mauaji ambaye yuko chini ya ulinzi kwa mahojiano na kwamba anazidi kuongeza vikosi vya doria kuimarisha ulinzi na usalama na kuwasaka wahalifu.

                          SORCE MWANAICHI

NYOTA WA MUZIKI WA INJILI MAREKANI AFIWA NA BABA YAKE MZAZI


Mwimbaji anayetamba na wimbo wake maarufu "Break every chain" Tasha Cobbs wa nchini Marekani amefiwa na baba yake mzazi askofu Fritz Cobbs katika taarifa ambayo ilitolewa na mwimbaji mwingine wa injili nchini humo James Fortune kupitia mitandao ya kijamii kwakuwataka wapenzi wa muziki wa injili kumkumbuka katika maombi mwimbaji huyo kwakuwa amefiwa na baba yake mzazi.

Aidha kwa upande wake Tasha hakuandika chochote kuhusu msiba huo isipokuwa amewashukuru mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kwa maombi yao na kumalizia kwakuwaambia kwamba anawapenda.

WATATU MATATANI KWA MAKOSA TOFAUTI LIKIWEMO LA DITRICK SWADIKO KUTUHUMIWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MINNE


RPC -MUNGI
MWANDISHI ,DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
  
JESHI la polisi mkoani Iringa linawashikirilia watu wawili kwa makosa mawili tofauti likiwemo la Ditrick Swadiko (18) mkazi wa Ndiuka kata ya Ruaha kumbaka mtoto  wa miaka 4.

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea tarehe 20 januari majira ya saa 4 na nusu usiku.
 
Mungi alisema mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto Khadija ambaye ni mwanafunzi wa awali katika shule ya msingi Ndiuka na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

Na katika tukio jingine, Askari polisi wakiwa doria eneo la Mlandege walimkamata Isaya Kimota (27) mfanyabiashara na mkazi wa  Ipogoro manispaa ya Iringa kwa kosa la kukutwa na bangi.

Kamanda Mungi alisema tukio hilo lilitokea tarehe 20 januari majira ya saa 5 kamili usiku ambapo mtuhumiwa huyo alikutwa na bangi gramu 200 aliyokuwa ameihifadhi katika bahasha ya kaki.

Mbali na matukio hayo mawili tofauti, Kamanda Mungi alisema huko maeneo ya Lugalo kata ya Gangilonga manispaa ya Iringa, watu wasiojulikana waliiba pikipiki aina ya Sunlg yenye namba za usajili T 969 CEQ yenye chases namba LBRSPJB53C901897 yenye thamani ya shilingi 200,000,000/= ambayo ni mali ya Calist Tairo, watuhumiwa wanatafutwa.

VIJANA WA BODABODA WAFANYA KUFURU MBEYA




Mch Edward  mseve wa kanisa T.A.G ushirika wa uyole  amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na vijana ambao ni waendesha bodaboda  baada ya kuvuruga utaratibu wa ibada maalum ya mazishi katika kanisa hilo siku ya leo
Hayo yametokea baada ya kijana mmoja ambaye ni mwendesha bodaboda alifahamika kwa jina la Gabriel Ngalele kufariki dunia  na mch mseve kuanza ibada ya mazishi kanisani
Wakati ibada inaendelea vijana ambao ni waendesha bodaboda wapatao 300 walivamia kanisani hapo na kuchukua mwili wa marehemu huyo kwa nguvu na kuupeleka sehemu ya makaburini kwa ajiri ya  maziko 
Aidha vijana hao Wakiwa makaburini   waliendesha ibada   na hatimaye kuuzika mwili huo
Mch mseve ameeleza kuwa wengi wa vijana hao walikuwa walevi na wavuta bangi   kwani baada ya kuwatuliza vijana hao waache kupiga kelele wakiwa kanisani kwa ajiri ya maombi walianza kuhamaki na    kitu ambacho amedai kuwa huenda ndo kimechangia kuichukua maiti hiyo bila kufuata utaratibu
Mch huyo ameongeza kuwa hawezi kuchukua hatua zozote kwani hawajamdhulu kwa lolote huku akinabaisha kuwa hayo yote amemwachia mungu ashugulike na suala hilo
Hata hivyo kwa upande wake wa jeshi la polisi mkoani mbeya lilijaribu kutuliza kitendo hicho lakini lilishindwa kuwadhibiti vijana hao   kutokana na wingi wa mabodaboda  hao.

BAADA YA KAZI NZITO 2013, KWETU PAZURI WAPONGEZANA

Sarah Uwera mmoja kati ya solo hodari wa Ambassadors akiwa katika pozi.
Baada ya kazi nzito ya utumishi waliyoifanya mwaka jana, kwaya ya mabalozi wa Yesu ama waite Ambassadors of Christ wanaofahamika zaidi kwa album yao ya Kwetu Pazuri kutoka nchini Rwanda, waliamua kuwa na siku ya kipekee kwa wanakwaya wote kwenda ufukweni kupongezana kwa kazi ya kumuhubiri Kristo wanayoifanya.

Katika pikiniki yao iliyofanyika ufukwe wa Rwesero huko nchini kwao, walishinda pamoja wakipeana shuhuda, kula pamoja, michezo pamoja na uimbaji ambapo uongozi wa kwaya hiyo uliwapa vyeti vya heshima baadhi ya wanakwaya wa kwaya hiyo kwa utumishi wao wa kumuhubiri Kristo kupitia kwaya hiyo. Ambapo pia kwaya hiyo ilitumia muda huo kutiana moyo wanakwaya wote tayari kwa kumtangaza Kristo kwa mwaka 2014


Twendeni mabalozi tukapunge upepo.
Mandhari saaafi.
Picha ya pamojaaa.

Sijajua haya matofali yanawekwa chiniii ama yanataka kurushwa mwe!
MWAKA WA NEEMA KWA MATHA MWAIPAJA PAMOJA NA MMEWE JOHN SAIDI 
 MUNGU AMEWABARIKI MTOTO WA  KIUME WIKI HILI AMEJIFUNGUA SALAMA BILA OPARESHENI UTUKUFU KWA MUNGU.

        Matha mwaipaja siku ya send off yake akiwa na mumewe mchungaji john said.

Mwimbaji wa nyimbo za injili matha mwaipaja anayetamba na  albamu mbalimbali kama vile Ombi langu kwa Mungu na kwa msaada wa Mungu, wiki hii ya tare. 7 januari 2014 Mungu alimsaidia kujifungua mtoto wa kiume.

MKOA WA IRINGA WAJISIFU KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI MWAKA 2013

Wanahabari   wakiwa katika  kikao  hicho  leo
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Dr  Christine Ishengoma  akizungumza na wanahabari  leo  juu ya utekelezaji  wa Ilani  ya uchaguzi kwa  mwaka 2013
Wanahabari  wa  vyombo  mbali mbali  wakifuatilia  kikao  cha  Rc  Iringa
Wakuu  wa  idara   wakiwa  katika  kikao  cha  mkuu wa  mkoa  na  wanahabari  leo
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Dr  Christine Ishengoma  kulia  akieleza  jinsi ambavyo  mkoa ulivyotekeleza  ilani ya  uchaguzi kwa mwaka  2013

SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa leo imetoa taarifa ya  utekelezaji  wa Ilani ya uchaguzi  kwa mwaka 2013 huku ikijivunia mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa.

Akitoa taarifa   hiyo  leo mbele  ya  wanahabari  mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma alisema  kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo mkoa  wa Iringa  unajivunia ni katika sekta  ya  elimu, miundo mbinu, kilimo ,afya  na  nyingine nyingi.

Kwani  alisema  kuwa mkoa  umepiga  hatua  katika ujenzi  wa nyumba  za  walimu katika Halmashauri  zote za mkoa  wa Iringa lengo  likiwa ni  kuendelea  kuboresha  kiwango  cha  elimu  katika mkoa.

Akielezea  kuhusu  sekta ya afya  alisema kuwa hadi  sasa Hospital mbili  zinaendelea kujengwa katika manispaa na Kilolo pia  vituo  vya afya  na  nyumba  za watumishi  wa afya ikiwa ni  pamoja na kuendelea kusambaza  dawa katika vituo  vya afya.

Mkuu  huyo  wa mkoa  alisema  pia kumekuwepo na ufuatiliaji  wa huduma  zinazotolewa katika  vituo  hivyo na  Hospital .

KIKAO CHA CHANGIA TIMU YA LIPULI FC CHAFANYIKA ,WAJUMBE WATOA YA MOYONI

Wadau  wa Lipuli Fc  kutoa taasisi  mbali mbali  kutoka taasisi  za  kifedha
Mlezi  wa  timu  ya  Lipuli Fc Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma  akifuatilia kikao  hicho
Mlezi  wa  timu ya  Lipuli Fc mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akifungua kikao  cha changia  Lipuli Fc
/> Wazee  wa  timu ya  Lipuli Fc  wakiwa  katika  kikao hicho
MKUU wa  mkoa  wa  Iringa  Dr Christine  Ishengoma  ameanza kutembeza  bakuri  kwa  ajili ya  kuichangia  timu  ya  Lipuli Fc inayohitaji  kiasi cha zaidi  ya  Tsh  milioni 28 ili  kufanikisha   timu  hiyo  kuendelea na  ligi  daraja  la kwanza hatua  ya pili.
Huku  akiwabana  viongozi  wa  timu  ya  Lipuli Fc  kuanza  kueleza akiba ya  fedha  ambayo wanayo hadi  hivi  sasa kabla ya  kuanza  kuchangia wadau na kuwataka  kuwa na mikakati endelevu ya  kuweka akiba ya pesa.
Wakichangia  katika  kikao  hicho wadau  wa  soka  walitaka viongozi  wa  timu ya  Lipuli Fc  kuonyesha umakini katika kuichangia   timu  hiyo kwa kueleza  mapato na matumizi  ya  fedha  na  kuwa na utaratibu  mzuri  wa  kuichangia timu  hiyo.
Katibu  wa  timu  hiyo  Wilye  Chikweo alisema  kuwa  usajili wa  timu  hiyo  utatumia  kiasi cha Tsh milioni  4  wakati kambi  ya  timu  itatumia Tsh milioni 10 pia  mipira  20  kwa  kila mpira  Tsh 50,000 pamoja na mahitaji  mengine  yakiwemo ya marekebisho ya  uwanja Tsh 200,000
Hata  hivyo  alisema  kuwa  hadi  sasa  timu  hiyo ina akaunti  namba 01J207225200 Lipuli Football club   benki  ya CRDB .
Kwa  upande  wake  mwenyekiti wa  chama  cha mpira  wa miguu mkoa  wa Iringa Eliud Mvella Wamahanji  alisema  kuwa klabu  hiyo ya  Lipuli Fc  kuwa ina tatizo kubwa .
Alisema  kuwa  ni kweli  utaratibu wa Lipuli Fc katika  kuendesha   timu  hiyo haujatumika vema .
Wamahanji  alisema  kuwa  timu  hiyo inahitaji kucheza na kusafiri  ila bado  timu  hiyo imekuwa ikiendeshwa  kiugumu ugumu kutokana na kukosa  fedha.
“pamoja na mapungufu  ambayo  timu  inayo bado  viongozi  hao wa Lipuli FC imekuwa  ikijitahidi  kuendesha   timu  hiyo na kweli  ninawaoba  sana  kuichangia  timu  ya  Lipuli Fc  ili  kuweza  kusonga  mbele  zaidi mfano CRDB wanaweza  kusema  watachangia milioni 15 na  wengine  wakachangia  milioni japo 10 kwa  kila mmoja”
Kwa  upande  wake  mlezi  wa  timu  hiyo mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Dr Ishengoma  alisema  kuwa hadi  sasa tayari  amefanikisha  timu  mbali mbali kusonga  mbele  katika  mikoa ambayo amepata  kufanya kazi ukiwemo mkoa  wa Ruvuma na Pwani  na kuwa  hadi  sasa bado mkoa  wa  Iringa.
Hata   hivyo  aliwataka   wadau  wa maendeleo  katika mkoa  wa  Iringa  kujitokeza  kuichangia  timu  hiyo ya  Lipuli Fc kama  sehemu ya  kufanikisha  kuutangaza  mkoa  wa Iringa kama  ulivyo mkoa  wa Mbeya na mikoa mingine ambayo imefanikiwa  kimichezo.
Pia  aliwataka  wanaotaka  kuisaidia  timu  hiyo ya  Lipuli Fc kuingiza michango  yao katika akaunti ya timu  iliyopo CRDB akaunti  namba 01J207225200 Lipuli Football club.
...................................................................................................................
...............................

MKAZI  wa Kijiji cha Ihowanza  wilaya  ya  Mufindi mkoani Iringa John Nwali (40)  akutwa amekufa baada ya kutoweka nyumbani  kwake kwa  wiki  moja   mara  baada ya  shamla  shamla  za kuuaga  mwaka mpya 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo leo alipokuwa akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake.

Alisema  kuwa tukio hilo lilitokea Januari 9 majira ya saa 1 jioni mwaka huu katika Kitongoji cha Ihowanza Kata ya Ihowanza Tarafa ya Malanali Wilaya ya Mufindi.

Alisema  mwili  wa  mkazi  huyo  ulikutwa  janurai 9 majira ya  jioni huku mwili wake ukiwa umeharibiwa vibaya  na baadhi ya viungo vyake kuliwa na mbwa na kuwa  jeshi la  polisi linaendelea na uchunguzi zaidi  juu ya  kifo  hicho.

JAMANI MANABII NA MITUME KWELI HAYA NDIO MAOMBI KULA MANYASI? MWE WAPENDWA KUWENI MAKINI

Mdada akila majani ambayo huduma hiyo wanasema ni chakula kutoka mbinguni mwe!
Kuna mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi mbalimbali, moja wapo ni hii huduma iitwayo Rabboni Centre ministries iliyopo Pretoria nchini Afrika ya kusini, huduma hii iliyochini ya mwanzilishi wake mwalimu ,mchungaji na nabii Daniel Lesego ilianza mwaka 2002. Ni huduma ambayo kwa watu wasioabudu hapo huitilia mashaka kutokana na mwenendo wake.

Kwasasa wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na hatimaye wanaishia kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo akisema kwamba Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.


Inaelezwa kwamba mara baada ya maombi waumini wengi huanza kutapika jambo ambalo kanisani hapo huashiria kwamba mtu amejazwa Roho Mtakatifu.


Lakini kama haitoshi nabii Lesego hufanya maombi huku amewakanyaga watu. Huduma hii imekuwa gumzo nchini humo na nchi jirani kwa jinsi mambo yao yanavyokwenda.


Mnasemaje watumishi kuhusu jambo hili? mwe kula manyasi kweli? mma!


Hapa nabii huyo akikanyaga watu kama njia ya mafundisho yake.
Haa!! angalia jamani, sasa ng'ombe watakula nini jamani???
Mungu tufunulie macho ya rohoni kuyajua mambo haya kama ni wewe au sisi kha!
Hajamaliza bado.
Baada ya manyasi ni mwendo wa kutapika sasa

SHORT HISTORY ABOUT WILLIAM MGIMWA

William Augustao Mgimwa (20 January 1950 – 1 January 2014) was a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Kalenga constituency from 2010 to 2014. He also served as Tanzania's Minister of Finance from 2012 to 2014.[1]

Early life and career

He was educated at Mafinga Seminary and Tosamaganga Seminary schools. He thereafter joined the Institute of Finance Management and the Institute of Development Management (present day Mzumbe University) for his MBA in finance.
He had worked at the National Bank of Commerce as an accountant and was the principal of the Bank of Tanzania Training Institute in Mwanza from 2000 to 2010. He was elected by a landslide in 2010 as the member of parliament for Kalenga constituency, receiving 31,421 votes (84.39%). In May 2012, President Jakaya Kikwete appointed him as the Minister of Finance.

Death

He died on 1 January 2014 at Kloof Medi-Clinic in Pretoria, South Africa where he was undergoing treatment.[2][3] His body is expected to be repatriated to Dar es Salaam on 4 January and will lie in repose the next day at Karimjee Hall. He will be buried at his home village of Magunga in Iringa Region.[4]

Publications

  • W. Mgimwa: Liquidity Management, Tanzania Bankers Journal, Dar Es Salaam. 1994
  • W. Mgimwa: Commercial Bank Lending Journal, Dar Es Salaam. 1995
  • W. Mgimwa: Advanced Credit Operations, Dar Es Salaam. 2007
  • W. Mgimwa: Advanced Treasury Management, Dar Es Salaam.

References

  1. Jump up ^ "Member of Parliament CV". Parliament of Tanzania. Retrieved May 2012.
  2. Jump up ^ "Finance Minister Dr Mgimwa dies in SA". IPP Media. 2 January 2014. Retrieved 2 January 2014.
  3. Jump up ^ "Mgimwa dies in South Afric". The Citizen (Tanzania). 2 January 2014. Retrieved 2 January 2014.
  4. Jump up ^ http://www.mof.go.tz/mofdocs/news/latest%20news/OFISI%20YA%20WAZIRI%20MKUU.p
SIKILIZA OVERCOMERS RADIO 98.6  KATIKA KUFAHAMU  NINI KINAENDELEA KUTOKA KATIKA JIJI CHA MAGUNGA AMBAPO MH.RAIS KIKWETE ANAONGOZA MAZISHI YA DR. MGIMWA

MAN UNITED MWAKA WA TABU, YATOLEWA KOMBE LA FA, YAPIGWA 2-1 NA SWANSEA

MIKOSI imeendelea kwa kocha David Moyes, baada ya Manchester United kufungwa mabao 2-1 na Swansea katika Raundi ya tatu ya Kombe la FA na kutolewa.
Bao lililoizamisha United iliyocheza pungufu ya mchezaji mmoja lilifungwa na Wilfried Bony dakika ya mwisho na Mashetani Wekundu wa wanatolewa katika raundi ya tatu kwa mara pili ndani ya miaka 30.
Javier Hernandez aliisawazishia United dakika ya 17 baada ya Wayne Routledge kuifungia Swansea bao la kuongoza dakika ya 12.
Shujaa: Bony akishangilia baada ya kuifungia Swansea bao lililoipeleka raundi ya nne ya Kombe la FA
Perfect: Bony rose above the United defence to head home Wayne Routledge's left-wing cross
Bony akiruka dhidi ya mabeki wa United kufunga

Katika mchezo mwingine, Liverpool imeifunga mabao 2-0 Oldham na kusonga mbele mabao ya Iago Aspas dakika ya 54 na Tarkowski aliyejifunga dakika ya 84.
The opener: Iago Aspas gave Liverpool the lead against Oldham in the 54th minute
Bao la kwanza: Iago Aspas akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza

BALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA WAZIRI MGIMWA...!!

WAKATI kukiwa na maswali mengi juu ya nini kilichosababisha kifo cha Waziri wa Fedha na Uchumi, marehemu Dk. William Mgimwa, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya amesema kifo chake ni cha kawaida na kimetokana na viungo vyake kushindwa kufanya kazi.
Balozi Msuya ametoa kauli hiyo

"Tundu Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga Ajitokeze".....Zitto Kabwe..!!

====Huu  ni  ujumbe  wa  Zitto Kabwe  kujibu  mapigo  ya  Tundu Lissu===
**
Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini. 

 Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.

 Nadhani alimwambia pia kuwa
Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.

Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over. Chacha died, I won't.

Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili.

RATIBA YA PILI YA MAZISHI YA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA HII HAPA



                                Dr  Wiliam Mgimwa  enzi  za uhai  wake 

Ratiba ya Mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Marehemu Dkt. William A. Mgimwa
Siku & Tarehe
Muda
Tukio
Mhusika
Jumamosi
4 Januari, 2014
 7:30
Mwili kuwasili JNIA
7:30 – 7:40
Kuutambua mwili na kukamilisha taratibu za uhamiaji
Bwana Bunare wa HAZINA na Mwanafamilia
7:30 -  7:40
Kumpokea mjane kutoka kwenye ndege kwenda VIP
Kaimu Waziri wa Fedha; Mwenyekiti wa Kamati; Mhe. Sophia Simba; Katibu Mkuu NJE; Balozi wa Tanzania Afrika ya Kusini; Monica Mwamunyange; Wanafamilia watatu
7:40 – 8:00
Mwili kubebwa na kuwekwa kwenye gari
Waombolezaji
8:00 – 8:30
Msafara kuelekea nyumbani
Kamati
8:30 – 10:00
Ibada ya Misa Takatifu nyumbani
Padre
10:00 – 10:30
Mwili kupelekwa Hospitali ya Lugalo
Kamati na Familia
10:30 – 12:00
Viongozi wa Kitaifa kutoa pole kwa familia
Mhe. Janeth Mbene na Kamati
Jumapili
5 Januari, 2014
2:00 – 4:00
Kifungua kinywa nyumbani kwa marehemu
Kamati
4:30
Waombolezaji kuwasili Viwanja vya karimjee
Kamati na Wanafamilia
5:00
Mwili kuwasili viwanja vya Karimjee
Kamati
5:45
Mhe. Makamu wa Rais kuwasili Karimjee
Kamati
6:00
Mhe. Rais kuwasili Karimjee
Kamati
6:00 – 6:20
Ibada fupi
Padre
6:20 – 6:25
Wasifu wa marehemu
Katibu Mkuu – HAZINA
6:25 – 6:30
Salamu za rambi rambi
Waziri wa Fedha wa Uganda kwa niaba ya Mawaziri wa Fedha Afrika Mashariki
6:30 – 6:35
Salamu za rambi rambi
Mwakilishi wa Washirika wa Maendeleo (DPs)
6:35 – 6:40
Salamu za rambi rambi
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kwa niaba ya Vyama vya Upinzani
6:40 – 6:45
Salamu za rambi rambi
Kiongozi wa CCM Bungeni
6:45 – 6:55
Salamu za Bunge
Spika wa Bunge
6:55 – 7:00
Salamu za rambi rambi
Waziri wa Fedha, Zanzibar
7:00 – 7:05
Salamu za rambi rambi
Kaimu Waziri wa Fedha SMT
7:05 – 7:10
Shukrani
Mwakilishi wa Familia
7:10 – 7:15
Hitimisho
Mwenyekiti wa Kamati
7:15 – 8:00
Kutoa Heshima za mwisho
Kamati
8:00 – 8:40
Kuelekea Uwanja wa Ndege
Wanaosafiri
10.00-11.00
Mwili kuwasili uwanja wa ndege wa Nduli Iringa na kuelekea katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo kwa heshima za Mwisho
Mkuu wa Mkoa na Kamati
11.00
Mwili kuelekea Kijijini Magunga

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog