Home » »

Baada ya kununua nyanya za kopo Supermarket, kufungua ndani kilichokutwa ndani ni ishu yani !!

lizad

Pata picha unaingia zako supermarket, unanunua mahitaji mbalimbali ya jikoni na unabaki na hesabu moja tu nyepesi kwamba ukifika home kazi yako ni kupika, alafu unakuja kufungua unakutana na vitu vya ajabu.
Muhammad Hussain na mkewe Sanam wanaishi Birmingham, Uingereza.. Walitoka zao Supermarket na vitu mbalimbali walivyonunua, kuja kuingia jikoni kwa ajili ya kuandaa chakula mwanamke huyo akakuta ndani ya kopo la nyanya kuna mjusi aliyekufa.
lizad2
Pamoja na kupeleka malalamiko yao kwa uongozi wa Supermarket hiyo inayoitwa Masala Bazaar waliombwa radhi kwa kitendo kilichotokea, wakaahidiwa kwamba kutafanyika uchunguzi jinsi gani imetokea mpaka mjusi huyo kaingia ndani ya kopo hilo ambalo ni ka nyanya ambazo zimesindikwa toka Italy.
lizard4
Mke wangu alikuwa jikoni anaandaa chakula cha mchana, nikasikia anapiga kelele.. kwenda nikakuta ndani ya kopo hilo la nyanya kuna mjusi aliyekufa“– Muhammad Hussain.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog