UPENDO KILAHIRO NA CHRISTINA SHUSHO WAPO NCHINI CANADA KIHUDUMA


Baada ya kazi njema ya kumtukuza Mungu katika mkutano mkubwa wa injili nchini Canada ulioandaliwa na askofu Zachary Kakobe, waimbaji nyota wa gospel nchini Christina Shusho pamoja na Upendo Kilahiro bado wanaendelea na huduma ya injili nchini humo kabla ya kuelekea nchini Marekani kuendeleza moto wa injili.

Katika mawasiliano na GI,Upendo amesema wanamshukuru Mungu mkutano ulikuwa wa baraka sana, ambapo kwasasa wanajiandaa kwaajili ya tamasha kubwa la uimbaji tarehe 7/7/2013 huko Ottawa katika jengo la Wells of Salvation Church kwa anuani ya Venue 1401 Blair Place, tarehe 14 July wanatarajiwa kuwa katika mji wa Quebec. kisha wataelekea nchini Marekani. Waimbaji hao wamewakaribisha watu wote kutoka Afrika Mashariki na sehemu nyinginezo kufika katika mahali watakapohudumu.


Upendo Kilahiro ameachia album mpya hivi karibuni ikijulikana kwa jina la "Sinzog'igo Ntinya" huku Christina Shusho akiwa anaachia album nyingine iitwayo "Nataka Nimjue", waimbaji hao kwa pamoja wamekuwa wakifanya vizuri katika tasnia ya muziki wa gospel nchini kwa muda mrefu ikiwa pamoja na kupata mialiko mingi ndani na nje ya nchi.



OMBI LANGU KWA MUNGU YA MATHA MWAIPAJA DVD KUPATIKANA MADUKANI KOTE SASA KUNZIA MWEZI HUU WA SITA

                                             Matha mwaipaja katika pozi
Baada ya kukaa kwa muda mrefu tangu kutoka kwa audio cd ya ombi langu kwa mungu hatimaye video yake imekamilika na ipo madukani kote tanzania akizungumza na mtandao huu matha mwaipaja ambye sasa anawania tuzo za AGMA nchini  london zitakazo tolewa mwezi wa saba amesema wapenzi wake wa mziki sasa watamuona laivu kupitia video cd watayoinunua ambayo ina nyimbo zenye ujumbe wa kuwaponya na kuwafungua watu

GOSPEL ZA IRINGA NA HABARI

KWA TAARIFA YAKO : MASWALI MENGI KUHUSU NDOA YALIMFANYA MARION SHAKO KUDANGANYA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina ukweli utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo kwa mwanadada aliyetokea kuteka masikio ya wakazi wa Afrika Mashariki kupitia wimbo wake "AHADI ZAKE" uliomtambulisha vyema na kumpatia tuzo huko nchini kwao Kenya, huyu si mwingine bali ni Marion Wyali Shako.

KWA TAARIFA YAKO kama ukuwahi kufahamu hili au kusoma makala tuliyowahi kuandika kuhusu mwimbaji huyu na wimbo wake wa huo ambao wengi waliousikia mara ya kwanza walidhani mwimbaji ni Beatrice Muhone ni kwamba, kupitia Wapo Radio Fm akihojiwa katika kipindi cha ''Safari ya jioni'' alisema wimbo wa AHADI ZAKE ambao upo ndani ya album yake ya ''MSAADA WANGU'' alipewa neno la kinabii na nabii Teresia Wairimu kwamba Mungu atampa wimbo utakaobadilisha maisha yake na watu wengine,wakati anapewa unabii huo alikuwa katika hali ya uhitaji sana na album yake hiyo mpaka anaifanikisha kuirekodi ni Mungu mwenyewe alimsimamia kwani alimaliza salio lake lote alilokuwa nalo na pia alipitia mapito magumu sana.


KWA TAARIFA YAKO Marion Shako ambaye licha ya kuwa ni mwajiriwa pia anajihusisha na biashara huko kwao Mombasa Kenya  kutokana na kupata maswali mengi ya watu kila anakokwenda kuhudumu kuhusu lini ataolewa ilibidi adanganye kwenye moja ya shoo ya mchekeshaji maarufu wa Kenya aitwae Churchill ambako aliulizwa swali kuhusu harusi yake lini bila kusita Marion alijibu itakuwa hivi karibuni kitendo ambacho alijutia baadae kwakuwa alidhani amepunguza maswali kumbe ndio yalikuwa yameongezeka na watu kutaka kujua undani zaidi wa harusi yake itafanyika lini na ninani muhusika mkuu, kitendo cha kuulizwa sana maswali ikabidi aweke jibu hadharani kwamba hawezi kuzungumzia masuala yake ya uhusiano hadharani na kwamba hategemei kufunga harusi kwa mwaka huo(ilikuwa 2011, GK haijui kama amefunga kwasasa pia) na kusema kwamba aliamua kusema anafunga harusi karibuni ili kuwaridhisha mashabiki na watu waliokuwa wakimuuliza maswali hayo kwakuwa walitaka jibu kama hilo. kama alivyofafanua kwenye mahojiano na gazeti la The Star

MARTHA MWAIPAJA NA CHRISTINA SHUSHO NDANI YA LONDON, WAPIGIE KURA YAKO

MARTHA MWAIPAJA NA CHRISTINA SHUSHO NDANI YA LONDON, WAPIGIE KURA YAKO



Martha Mwaipaja nyota yake imeonekana kung'ara na kutambulika kimataifa baada ya kupendekezwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo za injili za Afrika ziitwazo Africa Gospel Music Awards(AGMA) ambazo zinatarajiwa kutolewa mapema mwezi wa saba mwaka huu jijini London.

Mwimbaji huyo anayetamba na album yake ya pili aliyoitoa mapema mwaka jana amewekwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya mwimbaji wa mwaka Afrika mashariki akiwa sambamba na nyota mwingine wa muziki wa injili nchini Christina Shusho ambaye amependekezwa kuwania tuzo hizo kwa mara ya tatu mfululizo. Waimbaji hawa pekee kutoka Tanzania watakuwa wanawania tuzo hiyo na waimbaji wengine kutoka Kenya na Uganda.
Christina Shusho.


Kama ilivyokuwa kwa mwaka jana ambapo blog za Kikristo nchini tuliendesha kampeni ya kumwezesha Shusho kutwaa tuzo hiyo lakini kura hazikutosha, kwa mwaka huu tunao waimbaji wawili kutoka
nchini, ukiwa kama Mtanzania na mwana Afrika Mashariki tunaomba chukua muda wako wa dakika zisizopungua tano kuwapigia kura waimbaji wetu.

Wanaowania tuzo ya mwimbaji wa mwaka Afrika mashariki ndio hawa

Eunice Njeri (Kenya)
Christina Shusho(Tanzania)
Jimmy Gait (Kenya)
Kambua (Kenya)
Jackie Senyonjo(Uganda)
Kris Eh Baba (Kenya)
Coopy Bly-Uganda
Martha Mwaipaja-Tanzania
DK Kwenye Beat(Kenya)
Eko Dydda(Kenya)

Hata hivyo katika tuzo hizo kama ilivyokawaida waimbaji kutoka nchini Kenya wameonekana kung'ara katika kuwania tuzo tofauti huku, kinyang'anyiro kikali kinategemewa kuwa kusini mwa bara la Afrika ambako waimbaji nyota wa Afrika ya kusini wanawania tuzo hizo pia. Ambapo katika kinyang'anyiro hicho mwimbaji nyota kutoka kundi la Joyous Celebration Charisma Hanekam anatarajiwa kuwa mmoja wa waimbaji siku ya kutolewa kwa tuzo hizo zitakazofanyika tarehe 6/7/2013 katika ukumbi wa The Great Hall, Queen Mary jijini London nchini Uingereza.

Kungalia vipengele mbalimbali vya tuzo na waimbaji waliopendekezwa ikiwa pamoja na upigaji kura BONYEZA HAPA

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog