KIZUNGUZUNGU YA ENOCK JONAS YAITIKISA IRINGA.
 

mwimbaji enock jonas katika picha


 
Ni ujio ,mpya wa mwimbaji wa nyimbo za injili tanzania enock jonas  umewatikiza wakazi wa nyanda za juu kusini baaada ya kuja na albamu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wakazi hao
akizungumza na mtandao huo mmoja kati ya wakazi wa iringa aliyenaswa na mtandao huu akinunua nakala ya albamu hiyo ya kizunguzungu amesema amevutiwa sana na uimbaji wa mwimbaji huyo huku akimsifia kuwa anatazama wakati tulio nao kwani watu wengi wametawaliwa na imani ya kifremasoni na hawaamini kuwa kuwa yesu ni mtaji anaweza kuwatajirisha na ndani ya albamu hiyo utakutana na nyimbo kali kama vile yesu ni mtaji ,nipe mdundo kizunguzungu na wimbo ambao watu wengi wapendezewa sana nao unaitwa ninafuta maneno yenu
MWIMBAJI MKONGWE WA GOSPEL NA MWIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA JENIFA MGENDI ALI MAALUFU DATI SASA KUJA KIVINGINE NA FILAMU MPYA ,ALBAMU MPYA, AKIWASHIRIKISHA WAIMBAJI WAKONGWE KAMA VILE MCHUNGAJI ABIUD MISHOLI.
                                                         JENIFA AKIWA KATIKA POZI
  





newz

Akizungumza na mmiliki wa mtandao huu hivi karibuni mwimbaji huyo amesema kuwa anatarajia kuingiza sokoni muda sio mrefu filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la MAMA MKWE Ambapo anasema tafsiri ya filamu hiyo inatokana na wimbo utakao beba jina la albamu yake inayokwenda kwa jina la NDOA NI MGODI.
Katika filamu hiyo amewashirikisha waigizaji mabalimbali wakiwemo BI.ESTA ,CHRISTINE MATAI,BAHATI BUKUKU,SENGA, Pamoja na mkali wa kutengeneza filamu Tanzania Musa Banzi na wengine kibaoooooooooooo
anasema kila kitu kimekamilika soonnnnnnnn itakuwa mtaani jiandae kujipatia copy yako sasa.


MCHUNGAJI PETER MSIGWA AENGULIWA KUWANIA UENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI

Add caption
KUELEKEA UCHAGUZI WA CHADEMA IRINGA MJINI: Habari zisizo rasmi kutoka eneo la chumba cha mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zimedai kwamba Mchungaji Peter Msigwa ameenguliwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti.

Ameenguliwa kwa kile kilichoelezwa na wapashaji wetu kwamba anachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza makundi ndani ya chama hicho.

Makundi hayo yanaelezwa kukiwekwa rehani chama hicho wakati kikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Pamoja na Mchungaji Msigwa, taarifa hizo zimesema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao (Chadema) naye ameenguliwa kuwani nafasi yoyote ya uongozi katika chama hicho mkoani hapa.

Hivikaribuni Abwao alinukuliwa akitangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa chama hicho unaotarajia kufanyika Jumapili keshokutwa.

Kuenguliwa kwa Msigwa katika uchaguzi huo kumeacha kampuni wagombea wawili wanaomenyana katika nafsi hiyo itakayosaidia kutoa picha ya jinsi mambo yatakavyokuwa wakati wa mchakato wa kumpta mgombea ubunge jimbo la Iringa Mjini mwaka 2015.

Wagombea hao ni Frank Nyalusi anayeelezwa kuwa ni mfuasi wa kufa na kupona wa Mchungaji Peter Msigwa na Mohamed Makuke ambaye ni mfuasi wa kundi la wengi linalodaiwa kumpinga Mchunngaji Msigwa.

Kundi linalojiita la wengi katika chama hicho limesikika likisema mara kwa mra kwamba tabia ya Mchungaji Msigwa ndani ya chama hicho inawaweka katika wakati mgumu wa kutetea nafasi ya ubunge mwaka 2015.

Mchungaji Msigwa ni kiongozi asiyeambilika, anayejua kila kitu, mbishi, kaidi, mwenye kiburi, asiyependa watu, mwenye visasi, majivuno na asiyetaka ushirikiano toka kwa wenzake, asiye na mikakati ya kujenga chama huku akiamini siasa za kitaifa pekee anazopenda zaidi zinaweza kulinusuru jimbo hili katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Wakati Mchungaji Msigwa akirushiwa lawama zote hizo, taarifa za uhakika zimedai kwamba ofisi ya wilaya ya chama hicho imefungwa na wameamuliwa kuondoka baada ya uongozi wa mbunge huyo unaomaliza muda wake kushindwa kulipa kodi ya pango. Mchungaji Msigwa ndiye Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Iringa Mjini anayemaliza muda wake hii leo.

Wanachama wa chama hicho wamechukizwa kwa hatua ya mbunge wao kuridhia kupoteza ofisi pekee ya chama hicho mjini Iringa kwasababu ya kushindwa kulipa Sh 540,000 walizokuwa wakidaiwa.

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangaza baadaye hii leo.

MAGAZETINI LEO VICHWA VYA HABARI

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

AJALI YA GARI YAUA WATU 6 NA KUJERUHU VIBAYA WENGINE 18 HUKO MKOANI RUVUMA

WATU sita ambao ni abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi kutoka Mbinga mjini kwenda makao makuu ya wilaya mpya ya Nyasa, mkoani Ruvuma wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa vibaya baada ya gari hilo walilokuwa wamepanda, kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Mihayo Msikhela, alisema gari hilo lenye namba za usajili T 759 BVR aina ya Nissan Civillian lilipata ajali Agosti Mosi mwaka huu, majira ya saa 10:30 jioni katika kijiji cha Burma kata ya Nyoni wilayani Mbinga.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akimtaka hali mmoja kati ya majeruhi Joseph Matembo aliyelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mbinga
Mihayo alifafanua kuwa ajali hiyo ilisababishwa na gari kuwa katika mwendo kasi, ambapo dereva aliyekuwa akiliendesha alishindwa kulimudu kwenye kona kali na hatimaye lilitumbukia katika shimo kubwa (korongo) na kusababisha mauaji na majeruhi hao.
“Mpaka sasa dereva aliyekuwa akiliendesha gari hili bado jina lake halifahamiki kutokana na kukimbia kusikojulikana, Jeshi la polisi tunafanya jitihada ya kumtafuta ili aweze kupatikana na baadaye tupate maelezo yakinifu juu ya tukio hili”, alisema Mihayo. 

Aliwataja walimu wa shule ya msingi waliofariki dunia kuwa ni Esther Kumburu wa shule Kilimani wilayani Mbinga na Efigenia Kayombe ambaye ni mwalimu wa shule ya Linda iliyopo Mbambabay wilayani Nyasa.
Vilevile kulikuwa na Ernest Ndunguru mkazi wa kijiji cha Mikalanga wilayani Mbinga, Anna Chitete kijiji cha Kilosa wilayani Nyasa na mmoja ambaye alifahamika kwa jina moja la Mbunda mkazi wa kitongoji cha Lusonga Mbinga mjini, na kwamba maiti moja ambaye ni wa kiume bado hajatambuliwa jina lake mpaka sasa.
Aidha Kamanda Mihayo alieleza kuwa maiti zote zimehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Mbinga, na kwamba majeruhi bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo lakini hali zao bado ni mbaya.
Hata hivyo alitoa wito kwa madereva wote mkoani Ruvuma, kuacha kuendesha vyombo vya moto barabarani kwa mwendo kasi, ikiwemo vile ambavyo vimekuwa vikibeba abiria kwani kufanya hivyo kuna hatarisha maisha ya watu wanaosafiri, kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwa uupande wake mkuuu wa wilaya ya mbinga Senyi Ngaga alipohojiwa na jamvilahabari kwa njia ya simu  kuhusina na ajali iliyotokea alieleza kuwa taarifa hiyo ameipata akiwa Jijini Dar es salaam kwa shughuli za kikazi lakini  hawezi kuongea chochote kwa sababu yupo nje ya wailaya hiyo.
“Mwandishi labda umtafute kaimu mkuu wa wilaya ambaye nimemwachia wilaya hiyo kwani yeye ndiye atakuwa na maelezo mengi ya wilaya hiyo ila sasa hivyo yupo mbeya kwenye mkutanao wa wawekezaji alisema Senyi”
Hata hivyo kaimu mkuu wa wilaya hiyo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya songea Joseph Joseph Mkirikiti alipohojiwa na jamvilahabari kwa njia ya simu alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo alidai kuwa  imetokea katika kijiji cha Burma kwenye eneo la mlima chunya ambapo gari hilo lilikuwa linatoka Mbinga kwenda Mbambabay.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog