BARCA RAHA TUPU KILA PEMBE YA DUNIA, ‘WAJILAMBIA’ KIBIBI CHA TURIN NA KUBEBA NDOO YA ULAYA…MWAKA WAO HUU
BARCELONA
imetimiza ndoto za kutwaa mataji matatu, baada ya kuifunga mabao 3-1
Juventus ya Italia Uwanja wa Olimpiki mjini Berlin Ujerumani na kubeba
Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo,
Ivan Racitkic dakika ya nne, Luis Suarez dakika ya 68 na Neymar dakika
ya 90, Barca ikirithi taji lililoachwa wazi na mahasimu wao, Real
Madrid.
Bao pekee la Kibibi KIzee cha Turin lilifungwwa na Alvaro Morata dakika ya 55.
Barca
ambayo tayari ina mataji ya La Liga na Kombe la Mfalme msimu huu,
ingeondoka na ushindi mtamu zaidi, kama bao lingine la Neymar
lisingekataliwa kwa madai aliunawa mpira kabla ya kufunga. Xavi alitokea
benchi na kwenda kucheza mechi yake ya rekodi ya 151 ya Ligi ya
Mabingwa akichukua nafasi ya Iniesta kipindi cha pili.
Kikosi
cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen, Alves, Pique, Mascherano, Alba,
Rakitic/Mathieu, Busquets, Iniesta/Xavi dk78, Messi, Suarez/Pedro dk90
na Neymar.
Juventus:
Buffon, Lichtsteiner, Barzaglia, Bonucci, Evra/Coman dk89, Marchisio,
Pirlo, Pogba, Vidal/Pereyra dk79, Tevez na Morata/Llorente dk85.

Safu hatari ya ushambuliaji ya watu watatu Barca; Luis Suarez, Messi na Neymar wakisherehekea na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment