MASIKINI..!! MWANAMKE HUYU AMWAGIWA MAFUTA YA MOTO USONI NA MKE MWENZA, KISA KIZIMA KIPO HAPA

Wakati chama cha
waandishi wa habari wanawake(TAMWA) kikilaani ukatili katika jamii
mwanamke mmoja mkazi wa Sokoine Road mjini Songea mkoani Ruvuma
Bi.Rehema Gwaya amefanyiwa ukatili na mke mwenzake kwa kumwagiwa mafuta
ya moto usoni na kuungua sehemu mbalimbali za mwili wake.
Bi. Rehema Gwaya ambaye
amelazwa katika Hospitali ya mkoa Songea akiwa na mwanae wa miezi saba
anasema chanzo cha kufanyiwa ukatili huo ni kutofautiana na mke mwenzake
aitwaye Zefania Chimgege baada ya kuhoji masuala ya usafi ambapo
Zefania aliyekuwa akipika maandazi akamwagia karai la mafuta ya moto
usoni.
Baada ya kufanyiwa
unyama huo shemeji yake ambaye ni mume wa Zefania Bw.Hafidh Hamidu Mbaya
akamwambia atoke nje ammalizie kwa kumchoma na kisu.
Mganga mfawidhi katika hospitali ya mkoa Songea(HOMSO) Dkt.Benedikt Ngaiza amesema amempokea mgonjwa huyo
Wakazi wa Songea wamelaani ukatili huo.
Rehema Gwaya na Zefania Chimgege wameolewa sehemu moja na wote wanaishi
katika nyumba ya baba Mkwe na waume zao na kwamba Zefania Chimgege
anashikiliwa na polisi kwa kufanya ukatili huo.
Via>>ITV
0 comments:
Post a Comment