BREAKING NEWS# WANAINCHI WATAKA KUZICHAPA NA POLISI KISA KUKAMATWA KWA M...

Mtoto wa miaka 14 alazwa hospital baada ya kung'atwa na panya.

HAKIMU AUAWA KWA KUKATWAKATWA NA MAPANGA

PIGO JINGINE TENA,YUSUPH MANJI ANYANG'ANYWA SHAMBA NA SERIKALI

UPTODATE #TUNDU LISSU HALI BADO NI TETE HAYA NDIYO MAENEO AMBAYO ALIPIG...

TAARIFA KTOKA KWENYE MAGAZETI LEO SEPTEMBER 13


MWINGINE APIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA DAR...RAIS MAGUFULI AMJULIA...

BREAKING NEWS ALIYEMWOMBEA KIFO TUNDU LISU AKAMATWA NA JESHI LA POLISI

KARIBU KUTAZAMA MAGAZETI YA LEO YA SEPTEMBER 10

Magazetini leo Jumatatu Septemba 11, 2017


Breaking news: Taarifa mbaya zaidi ya million 100 zatumika kuokoa uhai w...

BREAKING NEWS :TUNDU LISSU ATOA NENO ZITO KWA MWENYEKITI

WIMBO MAALUMU KWA MH: LISSU 'PRAY FOR LISSU' NEW SONG 2017

WIMBO MAALUMU KWA MH: LISSU 'PRAY FOR LISSU' NEW SONG 2017

BREAKING NEWS: MANJI AKATAA KUTUMBULIWA UDIWANI CCM

UKATILI:BINTI ABAKWA HADI KUFA NABODABODA

SPIKA WA BUNGE ATOA KAULI NZITO LEO BUNGENI KUHUSU LISSU

SIMBACHAWENE ATOA UTETEZI WAKE BAADA YA KUJIUZULU UWAZIRI

Aliyekuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , George Simbachawene ambaye amejiuzulu nafasi yake hiyo kufuatia agizo la Rais kuwataka watu waliotajwa kwenye ripoti ya Tanzanite na Almasi kupisha, amefunguka na kujitetea

Simbachawene amefunguka na kusema kuwa amehushishwa kwenye sakata hilo kwa kuwa alihudumu katika wizara hiyo na kusema lakini yeye hakuhusika kwa lengo la kuhujumu uchumi wa taifa wala hakuwa na lengo baya kwa nchi. 

"Kampuni ambayo ilikuwa na ubia na serikali iliamua kumuuzia mtu mwingine ili aje kufanya kazi na serikali kwa hiyo zilikuwa ni 'private arangement' ambazo lazima wazilete serikalini sasa hata kama angebaki yule wa mwanzo au huyu alichukua bila shaka matokeo ya kutokuwa na faida katika uendeshaji wa rasilimali hii yangekuwa ni yale yale, kwa hiyo uhusika wangu na kutajwa kwangu bila shaka ni kwa sababu nilihudumu kwenye wizara ile lakini nina imani ya dhati ya moyo wangu kwamba uhusika wangu haukulenga kuhujumu taifa, haukuwa wa maslahi binafsi bali ni katika majukumu ya kiutendaji" alisema Simbachawene 

Tangu Rais Magufuli ametoa kauli hiyo ya kuwataka wateule wake wote ambao wamehushishwa kwenye ripoti hizo mbili za madini zilizoundwa na Spika Job Ndugai kupisha ni mawaziri wawili wamethibitisha kufanya maamuzi hayo akiwepo Simbachawene pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ambandusi Ngonyani.

WANASHERIA KENYA WALAANI TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimelaani vikali tukio la kupigwa risasi Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu.

Rais wa LSK, Isaac Okero amesema tukio hilo limewashtua wanasheria wote wa Kenya.

“Tumepata taarifa kwamba Lissu amepigwa risasi akiwa kwenye gari lake mjini Dodoma, kwa kweli imetushtua sana na inahuzunisha,” amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

“Kwa pamoja tunalaani tukio hilo kwa kuwa hili limewagusa wanasheria wote wa Afrika na hata dunia kwa jumla. Tunasikitika kwa uvunjifu wa sheria uliofanyika,’’ amesema.

Amesema Lissu anafahamika kwa kutetea haki za binadamu, hivyo wanasheria wote wapo pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake na Mungu atamsaidia atarudi katika hali yake ya kawaida.

MAASKOFU KURUDISHA FEDHA ZA MGAO WA ESCROW

Askofu Msaidizi jimbo la Bukoba, Mhashamu Method Kilaini pamoja na Mhashamu Eusebius Nzigilwa wa jimbo kuu katoliki la Dar es salaam wamefunguka na kutoa taarifa kuwa wameamua kurudisha mgao wa fedha za Escrow ambazo walipewa na James Rugemalira.

Viongozi hao wa dini wamesema wameamua kurudisha fedha hizo za serikali kutokana na kuwepo kwa kesi mahakamani ya kuhujumu uchumi inayomkabili James Rugemalira ambaye ndiye aliwapa fedha hizo. 

Mhashamu Method Kilaini alidaiwa kupewa jumla ya fedha za kitanzania milioni 80.5 huku Eusebius Nzigilwa akidaiwa kupewa jumla ya milioni 40.4 

MANJI AJIZUIA KUTOA MACHOZI MAHAKAMANI

TAPELI WA MTANDAONI AKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA

TUNDU LISSU AMVAA WAZIRI WA MAGUFURI KUHUSU NDEGE

WATOTO WATATU WA LUCKY VICENT WALIOWASILI LEO WAWALIZA WATANZANIA WALIOENDA KUWAPOKEA UWANJA WA NDEGE WA KIA

Wazazi, watoto na watu mbali mbali wameshindwa kujizuia na kumwaga chozi walipokuwa wakiwapokea watoto Sadia Ismail, Doreen Eribariki na Wilson Tarimo, ambao wamerejea rasmi nchini wakitokea nchini Marekani walikokuwa wakipatiwa matibabu.
Watoto hao ambao ni manusura wa ajali iliyoua takriban wanafunzi 32 wa shule ya msingi Lucky Vicent, wamepokelewa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Anna Mghwira, Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, wazazi na wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent, waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Watu mbali mbali walihudhuria uwanjani hapo wakiwa na mashada ya maua kuwalaki huku kukiwa na burudani mbali mbali kutoka kwa sanii Mercy Masika wa Kenya, Angel Bernad wa Tanzania na Kwaya ya Shangwe kutoka jijini Arusha.

Shirika la Samaritan Purse la Marekani lilijitolea kusaidia watoto hao kuanzia usafiri na gharama za matibabu kwa muda wote ambao walikuwa nchini humo wakitibiwa, katika Hospitali ya Sioux City tangu mwezi Mei 15, kufuatia majeraha makubwa kwenye ajali kubwa waliyoipata tarehe 6 Mei 2017, wakitokea hospitali ya Mt. Meru Arusha.

Polisi Afrika Kusini wapiga kambi mipakani kumzuia mke wa Rais Mugabe





Maafisa wa polisi wa Afrika Kusini wametoa tahadhari dhidi ya Mkewe rais Mugabe katika mipaka ya taifa hilo , waziri wa polisi nchini humo amesema.
Ametuhumiwa kwa kumpiga na kumjeruhi mwanamke wa miaka 20 katika kichwa chake katika chumba cha hoteli karibu na mji wa Johannesburg .
Polisi wanatariaji kwamba Bi Mugabe mwenye umri wa miaka 52 alipaswa kujiwasilisha mbele yao siku ya JUmanne lakini akakataa kufanya hivyo.
Bi Grace mugabe kwa sasa hajulikani yu wapi lakini inaaminikwamba bado yupo Afrika Kusini.
Gabnriela Engels
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pia amewasili nchini Afrika Kusini kwa kikao cha viongozi wa mataifa ya Afrika Kusini SADC unaotarajiwa kuanza siku ya Ijumaa.
Bi Mugabe hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Waziri wa polisi Fikile Mbalula alisema: Sisi polisi wa Afrika Kusini tayari tumeweka notisi katika mipaka yetu yote ili kumzuia bi Mugabe kuondoka nchini siku ya Jumatano, wakili wa Afrika Kusini Gerrie Nel aliyefanikiwa kumshtaki mwanariadha mlemavu Oscar PIstorius anamuunga mkono mwanamke anayemtuhumu bi Mugabe kwa kumpiga, Gabriela Engels.
Bwana Nel sasa anashirikiana na kundi la Afriforum ambalo linapigania haki za Afrikaners nchini Afrika Kusini.
Kundi hilo limesema kuwa iwapo polisi watashindwa kuchukua hatua katika kesi hiyo basi litamshtaki bi Mugabe.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULY 13, 2017 - NDANI NA NJE YA TANZANIA


Magazetini leo Alhamis Julai 13, 2017 

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog