Home » »

Edward Lowassa, Dk. Bilal wachukua fomu za kugombea urais.


Mbunge wa Monduli Edward Lowassa mara baada ya kuchukua fomu  jana jioni.
 
Edward Lowassa katika ukumbi wa Nec makao makuu ya CCM Dodoma.
 
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa pamoja  na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wamechukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi .
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua Fomu mbunge wa Monduli  Edward  Lowassa aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika dftari la kudumu la wapiga ili waweze kupata haki yao ya kikatiba ya kupiga  kura.
 
Akijibu moja ya swali lililoulizwa kuhusu mpango kama akishindwa kuteuliwa kugombea urais Lowassa amesema kamwe hawezi kushindwa katika kinyang’anyiro hicho cha urais.
 
Kwa upande wake Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal alisema endapo atachaguliwa kuwa rais kupitia chama cha Mapinduzi atatekeleza vipaumbele  vifuatavyo;
 
-Kulinda misingi ya utaifa na kuimarisha umoja na uhuru
-Kuunusuru muungano ambao ni wa kipekee barani Afrika
-Kuwa na Tanzania Shindani
-Kusimamia miiko ya uongozi na utumishi wa umma
-Kuendeleza  ushirikiano na mataifa mengine.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog