Home » »

Ngeleja ajitosa urais,

Aja na vipaumbele vinne

aikimbia Escrow......Akana Kuvuliwa Uwaziri Kwa Kashfa.


MBUNGE wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais wa Tanzania, huku akiweka wazi kuwa yeye hakuhusika na kashfa ya Escrow kwa madai kuwa wapo watu wanaoitumia kashfa hiyo kwa lengo la kumchafua kisiasa.
 
Ngeleja alitangaza nia yake hiyo ya kuwania urais jana jijini Mwanza katika Ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu (BoT) , akiwa ameongozana na baba yake mzazi Mganga Ngeleja, mkewe Blandina na mtoto wa Shemeji yake Maria Ntanga.
 
Sakata la Escrow na maadili
Alisema kuwa wakati wa Sakata la Escrow yeye alichafuliwa na baadhi ya watu ingawa hakuweka bayana ni akina nani na kuongeza kuwa suala hilo lilitolewa ufafanuzi na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizungumza na wazee wa Dar es Salaam mapema mwaka jana.
 
“ Mimi katika suala la Escrow, Rais Kikwete alisema ni Sh bilioni 202 tu zilizobainika katika sakata la Escrow na kwamba zile hazikuwa fedha za umma bali ni za kampuni binafsi, katika hili kuna watu kwa makusudi wanaibua hasira za watu na kuwachafua wengine, wapo wanaotumia siasa kuchafua watu,” alifafanua.
 
Kuhusu kuvuliwa wadhifa wa uwaziri kwa ajili ya kubainika katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2012, alisema kuwa yeye hakuwa na kashfa kupitia ripoti hiyo na kamwe hakuondolewa uwaziri kwa sababu ya kashfa bali aliondolewa katika mabadiliko ya kawaida aliyoyafanya Rais Kikwete.
 
“Wapo watu wanaodhani katika mabadiliko ya mawaziri aliyoyafanya Rais Kikwete Desemba 4 mwaka 2012, sikuwa na kashfa yoyote ile, yalikuwa ni mabadiliko ya kawaida aliyoyafanya Rais Kikwete, hayakuwa ya kashfa kutokana na ripoti ya CAG,” alisema na kuongeza.
 
“Ndio maana leo hii nasimama kwa kujiamini mbele yenu, kama mtu anao ushahidi ajitokeze aseme hadharani kuwa mimi niliondolewa katika Baraza la Mawaziri kwa kashfa,” alisema.
 
Aja na vipaumbele vinne
Alisema endapo atachaguliwa kuiongoza Tanzania, Serikali yake itakuwa na vipaumbele vichache vinne vya kimkakati vitavyoiwezesha nchi iweze kufanikiwa na kufikia malengo ya kuwa taifa lenye kipato cha kati.
 
Alivitaja vipaumbele hivyo kuwa ni ujenzi wa uchumi imara, kuimarisha utawala bora, kuboresha huduma za jamii (elimu, afya na maji) na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji ikiwemo ya reli, bandari, barabara sanjari na kuiwezesha kuwa na umeme wa uhakika.
 
“Vipaumbele vyangu vikuu ni vinne, kujenga Uchumi imara; kipaumbele namba mbili ni Utawala Bora; kipaumbele namba tatu ni Huduma za Jamii (Elimu, Afya na Maji); kipaumbele namba nne ni Miundombinu kama reli, bandari, barabara na umeme wa uhakika,” alisema .
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog