Zaidi ya bidhaa zenye kilo 200 za dhamani ya mililion moja na nusu zimeteketezwa kwa moto na mamlaka ya chakula na dawa tfda nyanda za juu kusini


Mamlaka ya chakula na Dawa nyanda za juu kusini imeendesha zoezi la kuteketeza bidhaa mbalimbali mkoani iringa ambazo zimekwisha mda wake wa matumizi.


Akizungumza na nuru fm wakati wa kuteketeza bidhaa hizo Mkaguzi wa TFDA nyanda za juu kusini PAUL SONDA amesema kuwa wametekeza bidhaa hizo ili kulinda afya ya mlaji.

Aidha PAUL SONDA amewataka wanunuzi wa dawa au vipodozi kuhakikibidhaa hizo kwa kuangalia kama zimesajiliwa na TFDA.

Kwa upande wake AFISA AFYA Mkoa wa iringa HADIJAH HAROUN amebainisha kuwa ni vyema wananchi wakashirikiana na mamlaka husika kutoa taarifa kuangamiza
bidhaa ambazo hazijasajiliwa ili kulinda afya za wananachi.

DC KILOLO AMFUKUZA MKUU WA KITUO CHA POLISI MTITU .

                           NA DENIS NYALI IRINGA
Kufuatia kuripotiwa kwa wingi wa matukio ya ubakaji mkoani iringa na tanzania kwa ujumla mkuu wa wilaya ya kilolo  Mh Asia abdallah ameagiza kuhamishwa mara moja mkuu wa kituo cha mtitu kilichopo wilaya ya kilolo kutokana na uzembe wa kutofikisha taarifa za tukio la ubakaji kwa mkuu wa kituo cha polisi wilaya .

Tukio hilo limetokea baada ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano na nusu kubakwa na watu watatu katika kijiji cha mawambala na kuharibiwa vibaya sehemu ya mwili wake.
Akizungumzia Tukio hilo la kikatili lilotokea katika kijiji cha mawambala kata ya ukumbi wilaya ya kilolo mkoani iringa afisa mtendaji wa kijiji hicho NOLASCO KIHWELO  amesema taarifa juu ya tukio hilo zimelipotiwa na mama wa mtoto huyo.
Mtendaji wa kijiji ameongeza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo yeye pamoja na wazazi hao wakishirikiana kumkamata mtuhumiwa mmoja huku wengine wawili wakikimbilia kusikojulikana.
Akizungumza kwa uchungu mama wa mtoto huyo amesema alikuwa akipika jikoni ndipo baba mdogo wa mtoto huyo alipo mwona mtoto huyo akishindwa kutembea na ndipo mama yake alipofika na kumkuta tayari ameshafanyiwa ukatili huo.

NAYE  mtoto aliyefanyiwa ukatili huyo ambaye hajui lugha ya Kiswahili akizungumza kwa lugha ya kihehe amesema watuhumiwa waliotekeleza kitendo hicho walimtisha kuwa asimwambie mtu na endapo akisema watamkata kwa panga.

           

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog