Polisi Dar Wakamata Meno ya Tembo 156, Bunduki mbili


Rais Magufuli kamsimamisha mwingine Dec 22 2015




Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge"

Amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala yake imeonekana kutetea kilichofanyika

Aidha Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Benhadard Tito kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali vitakavyofanya uchunguzi zaidi kuhusu mchakato wa Zabuni hiyo.

Pia ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.

Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na jinsi bodi hiyo ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa ya treni.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
22 Desemba, 2015

Magazeti ya Tanzania December 23 2015 na stori zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho.



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Walichoongea Rais Magufuli Na Maalim Seif Baada ya Kukuta Ikulu Jijini Dar .


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana naMakamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad, leo tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam  kufuatia maombi yake ya siku nyingi.

Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi hawa kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea. 

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar. 

Rais Magufuli pia  amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar. 

Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif  Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane. 

Majadiliano yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema. 

Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar. 

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
21Desemba, 2015

Mbeya: Binti Akamatwa kwa Alichokiandika Facebook .

Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mtandao wa Face book.

Mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Carolne Kajela, alikamatwa jioni ya desemba 12, mwaka huu eneo la Uyole Jijini hapa, baada ya kuandika katika ukurasa wake wa Facebook kupitia kundi la Kwinyara Let’s talk kuwa, mmiliki wa mabasi ya Rungwe Express anaingiza mabasi hayo kupitia taasisi ya dini.

“Mtumbua majipu atumbue na hili.. mmiliki wa mabasi ya RUNGWE EXPRESS anapitisha mabasi kupitia taasisi moja ya kidin imbombo... jilipo,” unasomeka ujumbe huo, ambao mpaka anakamatwa ulikuwa umependwa na watu 35 na kuchangiwa maoni na watu 120

Taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na kuhojiwa, amekiri kosa na kuomba asamehewe kwani shetani alimzidi.

Mmiliki wa mabasi hayo Yohana Sonelo, alipohojiwa amekiri kampuni yake kupeleka mashitaka polisi na kwamba wanahitaji athibitishe alichokiandika mtandaoni, lasivyo sheria ya makosa ya mtandao namba 14 ya mwaka 2015 ambayo ilianza kutumika Septemba Mosi mwaka huu ifuate mkondo wake.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kumkamata mtuhumiwa huyo na kwamba taratibu za upelelezi zinaendelea kisha watapeleka jalada kwa mwanasheria wa serikali ili mtuhumiwa afunguliwe mashitaka na afikishwe mahakamani.

Magazeti ya Tanzania December 22 2015 na stori zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho.


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog