Home » »

Afungwa miaka 30 kwa kumbaka mtoto wa miaka tisa


Mkazi wa Malampaka mkoani Simiyu, Benedictor Bulobo (30) , ametupwa gerezani atakakotumikia kifungo kwa miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti wa miaka tisa.

 Alihukumiwa  na Mahakama ya Wilaya ya Maswa juzi na Hakimu Mwandamizi Mfawidhi  Agatha Chigulu, baada ya kuridhishwa  na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Akitoa hukumu hiyo hakimu huyo alisema kuwa anatoa adhabu hiyo ili kukomesha vitendo hivyo na kuwaonya wenye nia  mbaya ya kutaka kutenda kosa kama hilo wajifunze na kuacha mwenendo huo.

Chigulu alieleza kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 131 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.

 Awali mahakama iliambiwa na  Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Nassibu Swedy kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 23 mwaka jana  saa 5:00 asubuhi.

Alimnajisi mtoto huyo  maeneo ya nyumbani kwake baada ya kumkamata  kwa nguvu binti huyo mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Malampaka na kumwingiza chumbani kwake alipombaka.

Alisema mtoto huyo  alipata maumivu makali  baada ya kuumizwa  sehemu za siri,  alipiga kelele kuomba msaada na watu walifika katika eneo la tukio,  kumkamata  na kumfikisha Bulobo katika kituo cha polisi Malampaka.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog