Mtoto wa Miaka Mitatu Abakwa Na Kunyongwa Hadi Kufa.

Mtoto mwenye umri wa miaka 3 na miezi 4 Mariam Deogratius mwanafunzi wa shule ya awali ya Makoko iliyopo katika Manispaa ya Mji wa Musoma mkoani Mara, amebakwa kisha kunyongwa hadi kufa na mtu asiyejulikana Usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara kamishna msaidizi Philllip Kalang amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linafanya Msako kuhakikisha Mhalifu anapatikana.

Zimenifikia kurasa za mbele za magazeti ya Uingereza ya Leo February 24

 24.Screenshot_2016-02-24-02-39-29-1
Screenshot_2016-02-24-02-40-50-1
Screenshot_2016-02-24-02-40-56-1
Screenshot_2016-02-24-02-41-00-1
Screenshot_2016-02-24-02-41-05-1
Screenshot_2016-02-24-02-41-10-1
Screenshot_2016-02-24-02-41-29-1
Screenshot_2016-02-24-02-41-35-1
Screenshot_2016-02-24-02-41-39-1
Screenshot_2016-02-24-02-42-11-1
Screenshot_2016-02-24-02-43-11-1

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akana Kutoa Amri ya Kufuta Matokeo ya Uchaguzi Zanzibar .

 
 
 
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete amesema hajahusika kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kwa kumpigia simu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Aliyasema hayo juzi mjini Kibaha wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Chama ya Kibaha Mjini mkoani Pwani na kusema maneno hayo ni ya uongo, hayana ukweli wowote na watu hawapaswi kutoa shutuma hizo juu yake.

Rais huyo wa Awamu ya Nne alisema maneno hayo hayana kichwa wala miguu wala hajawahi kumpigia simu Jecha kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwani tume hiyo inajitegemea.

“Wasitoe lawama zisizohusika, wapuuzeni sikuwahi kufanya hivyo hata kwa Damian Lubuva wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania hivyo nashangaa watu wanavyosema kuwa nimehusika kufutwa uchaguzi huo,” alisema Kikwete.

“Tume ya Zanzibar ni tume huru na inajitegemea kwani ina mambo yake hata Dk Ali Mohamed Shein (Rais wa Zanzibar) hana uwezo wa kuingilia na kuahirisha uchaguzi huo, watu hao wasipake watu matope wasio husika kwani kila mtu ana nafasi yake,” alifafanua Kikwete.

Alisema kikubwa kinachotakiwa ni kuwaombea Wazanzibari wafanye uchaguzi wao mkuu wa marudio kwa amani na utulivu ili wapate viongozi wao wa kuiongoza Zanzibar na wawaombee wagombea wa CCM washinde.

Aidha, alisema chama hicho kinapaswa kuwaadhibu watu waliokihujumu chama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa kutomwonea mwanachama, bali watende haki na si kwa kwa uonevu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao alisema Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka ameonesha njia ya kiongozi kutumia fursa kuboresha mazingira ya utendaji kazi Awali, Koka ambaye ndiye aliyejenga ofisi hiyo yenye thamani ya Sh milioni 100, alisema aliamua kujitolea kujenga ofisi hiyo kwa lengo la kukisaidia chama kiendeshe shughuli zake.

Koka alisema aliamua kujenga kama kumbukumbu kwa wanaKibaha ili iwe kielelezo cha uongozi wake kama mbunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kufanya shughuli za chama badala ya kufanyia sehemu zisizo na hadhi yao.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano Ya Februari 24 .

Baba Amchoma Mwanawe vidole kisa Mboga Ya Sh. 500

 
MKAZI wa kitongoji cha Kazima – Kichangani Kata ya Kawajense, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Emmanuel Joseph (31) amemfanyia unyama mtoto wake wa kumzaa, George Emmanuel (4) kwa kuvichoma kwa moto vidole vyake vya mkono wa kushoto, akimtuhumu kukomba mboga yote ya majani aina ya ‘chainizi’ yenye thamani ya Sh 500.

Inasemekana baba huyo amekuwa akiishi na watoto wake watatu baada ya kuachana na mkewe wa ndoa, Semsni Jahala (28) Machi mwaka jana.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Rashid Mohamed amethitibisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema lilitokea juzi saa 12 jioni katika kitongoji cha Kazima– Kichangani.

Akisimulia mkasa huo, Kaimu Kamanda Mohamed alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa mahojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali wa shauri lake kukamilika.

“Jioni hiyo ya tukio saa kumi na moja jioni mtuhumiwa huyo (Emmanuel) alipika chakula cha jioni, ugali na mboga za majani maarufu chainizi kisha akakihifadhi chakula hicho jikoni na kuondoka … aliporudi nyumbani saa kumi na mbili jioni ili kuandaa chakula cha jioni ndipo alipobaini mtoto wake (George) amekomba mboga yote ya majani. 

"Alikasirishwa na kitendo hicho na kusababisha kumpiga kisha kumchoma moto vidole vyake vitatu vya mkono wa kushoto na kumsababishia maumivu makali,” alieleza Kaimu Kamanda.

Kwa mujibu wa mashuhuda kutoka eneo hilo la tukio, mtoto huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako amelazwa kwa matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda, Oscar Mkenda alisema mke aliamua kuachana na mumewe huyo baada ya kuchoshwa na ukatili na unyanyasaji aliokuwa akifanyiwa, ikiwemo kupigwa mara kwa mara bila sababu yoyote.

“Mtoto George alikomba mboga hizo zote za majani baada ya kushinda na njaa mchana kutwa kwani hata kifungua kinywa hakupa asubuhi… hivyo baada ya baba yake kubaini mtoto wake George amekomba mboga zote, ndipo alipochochea moto na kuukandamiza mkono wake wa kushoto na kuunguza vibaya vidole vyake vitatu,” alieleza Mkenda.

Kama ulikamatwa na Polisi barabarani Dar mwezi huu, faini yako imeijazia BILIONI MOJA kama ifuatavyo


Kikosi cha usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam kimetangaza kukusanya kiasi cha shilingi BILIONI MOJA NUKTA TISA (1.9) kutokana na faini za ukamataji wa makosa ya usalama barabarani kuanzia siku ya kwanza ya February 2016 mpaka tarehe 22 ya mwezi huu.
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema ‘Sio kwamba tunafurahia watu wafanye makosa ili tuingize pesa, hatupendi tuwe na pesa nyingi za makusanyo kwa ajili ya kuonea Wananchi… hapana, tunafanya hivyo kudhibiti na kuhakikisha kunakuwa na utii wa sheria‘

HIZO BILIONI 1.9 ZIMETOKANA NA HII LIST HAPA CHINI
  1. IDADI YA PIKIPIKI ZILIZOKAMATWA 4046
  2. IDADI YA MAGARI YALIYOKAMATWA 32528
  3. DALADALA ZILIZOKAMATWA 23,264
  4. MAGARI MENGINE (BINAFSI NA MALORI) 9264
  5. JUMLA YA MAKOSA YALIYOKAMTWA 36,574
Hii taarifa imekuja siku moja baada ya Wizara ya fedha kutangaza jana kukusanya mapato ya serikali na kufikia zaidi ya TRILIONI MOJA kwa mwezi February 2016 pekee ambao bado haujamalizika kikiwa ni kiwango tofauti na mwaka uliopita ambapo walikua wakikusanya kwenye BILIONI 800 n.k

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo February 17 2016 kwenye udaku, Hardnews na michezo

DSCN0363DSCN0408 DSCN0411 DSCN0365 DSCN0366 DSCN0367 DSCN0368 DSCN0369 DSCN0370 DSCN0371 DSCN0372 DSCN0373 DSCN0375 DSCN0376 DSCN0377 DSCN0378 DSCN0379 DSCN0380 DSCN0381 DSCN0382

PAA ZA NYUMBA NNE ZAEZULIWA NA UPEPO IRINGA.





Upepo mkali uliombatana na mvua kiasi umeezua paa za nyumba nne na kuwaacha wakazi zaidi 15 wakiwa hawajui jambo la kufanya mara baada ya kukumbwa na kadhia hiyo.
Familia hizo ambazo zipo Mtaa wa Nduli, Kata ya Nduli, Manispaa ya Iringa zimekumbwa na kadhia hiyo hii leo majira ya saa kumi na moja kasoro jioni ambapo hata hivyo hakuna mtu alipepatwa na dhoruba ya kupata majeraha ama kifo baada ya janga hilo.





Akizungumzia tukio hilo mara baada ya kufika na kujionea hali halisi, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Ndg Richard Kasesela ameuambia mtandao wa Wazo Huru kuwa, alipata taarifa hizo majira ya jioni ambapo aliamua kufika ili kujua ni kwa kiasi gani wakazi hao wamekumbwa na tatizo hilo.

Kasesela amesema ni tukio ambalo limemsikitisha kwa kiasi kikubwa kwani Mkoa huo bado upo katika maskitiko makubwa mara baada ya wakazi takribani 391 kutoka karibu kaya 99 kukumbwa na mafuriko katika Kijiji cha Kisinga, tarafa ya Pawaga yaliyosababisha serikali kutumia Helkopta kuwaokoa.

Kasesela amesema kuwa kesho asubuhi atatuma wataalamu kwa ajili ya kufanya tathimi ya kile kilichotokea ili kuona ni kwa namna gani serikali inaweza kusaidia wakazi hao ambao kwa sasa wamepatiwa hifadhi na majirani.

Kasesela amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani humo zimekuwa na changamoto kubwa kwa wakazi wa maeneo mbalimbali kutokana nakukosa makazi kwa sababu ya adha kubwa ambazo wamekuwa wakizipata, ambapo amesema serikali itajitahidi kukabiliana na kadhia yoyote itakayojitokeza ili kuwasaidia wananchi wanaokumbwa na matatizo yoyote.

Hata hivyo mkoa wa Iringa umeingia kwenye kadhia hii wakati zimepita siku chache tu mara baada ya vibanda 51 vya  wakulima wa mpunga kusombwa na maji katika vitongoji  vya Mboliboli na Kimande.

Aidha katika taarifa ya juzi iliyotolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi Amina  Masenza ilieleza kuwa serikali imefanya uchunguzi wa maji  katika mto Mlenge na katika  vyanzo vingine  vya maji kwenye tarafa ya Pawaga  ili  kuchunguza kama yana vimelea  vya Kipindupindu na kupitia  wataalam wa maji wa Bonde la Rufiji imebainika kwamba vyanzo vingi vya maji katika eneo hilo vina vimelea hivyo.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog