HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JULY 13, 2017 - NDANI NA NJE YA TANZANIA


Magazetini leo Alhamis Julai 13, 2017 

MZEE MWENYE WATOTO 100 ATAKA KUZAA ZAIDI ILI AZIKWE VIZURI AKIFA

Kofi Asilenu mwenye umri wa miaka 80 ni baba wa watoto 100 na wake 12.


Wakati ulimwengu ulipoadhimisha siku ya idadi ya watu duniani mwanaume mmoja alikuwa na sababu 100 za kusherehekea.
Kofi Asilenu mwenye umri wa miaka 80 ni baba wa watoto 100 na wake 12.
Anaishi na familia yake katika kijiji cha Amankrom kilicho umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu Acca.
Familia yake ni thuluthi moja ya watu 600 katika kijiji hicho.
Anasema kuwa anataka familia kubwa kwa sababu hana ndugu.
Sina kaka wala shangazi,ndiyo sababu niliamua kuwa na watoto wengi ndiyo wapate kunipa maziko yaliyo mazuri nikifa.
Familia hiyo yake hata hivyo imemgharimu pakubwa. anasema alikuwa mtu mwenye mali, lakini mali hiyo ilipungua kutokana na gharama ya kuitunza familia yake kubwa
Kofi Asilenu anaonekama kuwa mwenye afya nzuri na hata anasema anataka kuwa na watoto zaidi.
Via>>BBC

SERIKALI YAMWAGA AJIRA 10,184 KUZIBA NAFASI ZA WATUMISHI WENYE VYETI FEKI

 OFISI ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza kutoa vibali vya ajira 10,184 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais, Utumishi, Florence Temba, ilieleza kuwa agizo hilo linazihusu Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala wa Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma.
Ilimnukuu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akitoa agizo hilo wakati akizungumza katika kikao kazi na watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam jana.
“Mgawanyo wa vibali vya ajira umezingatia upungufu uliojitokeza baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki, vipaumbele vya Taifa kwa sasa na upatikanaji wa watumishi kutoka katika soko la ajira,” alisema Kairuki.
Kairuki aliongeza kuwa taratibu za kukamilisha mgawo wa nafasi za ajira 4,816 zilizosalia unaendelea ili kuwezesha wizara na taasisi nyingine zilizokamilisha uhakiki wa watumishi wa umma hivi karibuni kuajiri watumishi wapya kuziba nafasi wazi zilizojitokeza.
Alieleza kuwa serikali imetoa kibali kuajiri watumishi wapya 15,000 ili kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti baada ya zoezi la uhakiki.
“Watumishi wa umma watakaoajiriwa kuziba nafasi hizo wanatarajiwa kuripoti kazini kuanzia mwezi Agosti, 2017,” alieleza Waziri Kairuki, na kuongeza kuwa utaratibu wa ajira mpya za serikali upo palepale na amewataka wananchi kutokuwa na wasiwasi wowote wa ajira hizo.
“Napenda kusisitiza kuwa vibali tulivyovitoa leo ni vile vilivyoziba pengo la walioghushi vyeti, naomba wananchi watambue kuwa suala la ajira mpya bado liko pale pale kama serikali ilivyojipanga,” alisema Kairuki.
Aprili mwaka huu, Rais John Magufuli alipokea ripoti yenye orodha ya watumishi wa umma ambao kati yao wanadaiwa kuwa na vyeti pungufu, vyenye utata na vya kughushi kutokea kwa Waziri Kairuki.
Waliokuwa na vyeti vya kughushi walikuwa 9,932, na Rais aliapa kwamba hawatarudi kazini. Rais Magufuli aliagiza kufutwa kazi kwa wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo na kuzuia mishahara yao ya mwezi huo, lakini hata hivyo bado mlango uliwekwa wazi kwa wenye pingamizi na wapo waliokataa rufaa huku wengine wakienda kwenye mamlaka husika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.
Wiki iliyopita akiwa Dodoma, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alitangaza kuwa wiki hii serikali itatoa vibali 3,000 vya ajira katika sekta ya afya vikiwemo vya madaktari na wauguzi pamoja na maofisa hesabu 535 kwa ajili ya vituo vya afya vya kata ili washughulike na ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya afya na zahanati.
Chanzo-Habarileo

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog