Kesi ya Mauaji ya Mwanahabari, Daud Mwangosi Kuendelea Leo

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, jana iliahirisha kesi ya mauaji ya mwanahabari, Daud Mwangosi inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Iringa (FFU), Pasificus Simon hadi leo. 

Kesi hiyo iliahirishwa baada ya upande wa Serikali kufunga ushahidi wake. Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Februari 12, mwaka 2012, leo inaendelea kwa upande wa utetezi kuleta mashahidi wake mbele ya Jaji Paul Kihwelo anayeisikiliza.

Katika kesi hiyo ambayo haikuchukua muda mrefu mahakamani hapo jana, mawakili wa Serikali wakiongozwa na Sandy Hyra na Ladislaus Komanya walisema wamefunga ushahidi kwa mashahidi wanne wa awali.

Baada ya wakili wa utetezi, Rwezaura Kaijage kukubaliana na maombi ya upande wa Serikali kufunga ushahidi wao, Jaji Kihwelo aliiahirisha kesi hiyo hadi leo.

Awali, mtuhumiwa Simon alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ambao hawaruhusi apigwe picha na waandishi wa habari.

Mwangosi aliuawa kwa kupigwa bomu Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

DIWANI WA VITI MAALUMU CHADEMA KATA YA CHANGARAWE AZINDUA MAFUNZO YA MABADILIKO TABIA NCHI NA ATHARI ZAKED


               MATUKIO YA PICHA YA MAFUNZO YA MABADILOKO YA TABIA NCHI.
Mgeni rasmi Geogina kiduge wakati akikaribishwa meza kuu.


Mratibu wa mradi edson mwaibanje akitoa maelezo juu ya mradi huo















                            SOMA ZAIDI.

Jumla ya wanawake 85 kutoka katika kata za mji wa mafinga wilaya ya mufindi mkoani iringa wamenufaika na elimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza na DENIS NYALI BLOG  mratibu wa mradi wa mabadiliko ya tabia nchi na athari zake  ambao unafadhiriwa na WOMEN FUNDS,EDSON MWAIBANJE amesema wameamua kutoa elimu hiyo kwa wanawake kwa kuwa wana nafasi kubwa kuliko wanaume na ndio wamekuwa waathirika wa kwanza wa mabadilko ya tabia nchi.
                 
Aidha mratibu huyo amesema kutokana na jamii ya kimataifa kuelimisha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kupitia elimu ambayo wanawake hao wameipata itawasaidia kuelimisha wana jamii katika kata zao na kutafuta njia mbadala itakayo tumika kukabiliana na hali hiyo.
                    
Nao baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wameshukuru kwa elimu hiyo waliyopewa na kuahidi kuifanyia kazi huku wakielezea kuwa kwa sasa ratiba ya kilimo imekuwa haitabiliki kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

FPCT MANISPAA YA IRINGA WAZINDUA WIKI YA VIJANA KWA MICHEZO KATIKA UWANJA WA LUGALO MANISPAA YA IRINGA.


Timu ya vijana waliooa na wasiooa wakionekana katika picha kwa pamoja.


Timu ya mabinti ambao hawajaolewa wakiwa na wamama walioolewa


NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog