HAYA NDIO MATUKIO MUHIMU YA PAPA BENEDICT XVI

Papa Benedict wa 16, ameainisha wazi kuwa anastaafu uongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani mwishoni mwa mwezi huu, na hivyo kutoa nafasi kwa mchakatow a kumpata Papa mpya kuanza.

Yafuatayo ni matukio muhimu katika maisha yake, kama ambavyo GK imeyakusanya kwenye mtandao.

April 16, 1927: Kuzaliwa kwa Alois Ratzinger huko Marktl am Inn, Ujerumani, mtoto wa mwisho wa Joseph na Maria Ratzinger.

1943 - 1945: Amekuwa msaidizi wa majeshi ya ulizni nchini Ujerumani, kikosi cha kuzuia mashambulizi ya anga na askari wa miguu. Alifungwa jela mwaka 1945 kwenye kambi ya Wamarekani kwenye mji wa Neu Ulm, Bavaria, Ujerumani.

Juni 29, 1951: Akasimikwa rasmi sanjari na kaka yake, Georg Ratzinger huko Freising, Bavaria, Ujerumani.

1969 - 1977: Akawa Professa katika Chuo Kikuu cha Regesnburg, kilichopo Bavaria, huko huko Ujerumani.

Novemba 25, 1981: Akateuliwa kuwa kiongozi mkuu kwenye kusanyiko la kiimani linaloongozwa na Papa Yohane Paulo wa pili, na hatimaye kuchukua nafasi hiyo ilipofikia Machi 1892 akaichukua rasmi nafasi hiyo.

Aprili 2, 2005: Papa Yohane Paulo II anafariki dunia, siku sita baadae, yaani Aprili 8 2005, Ratzinger akiwa kama 'dean' wa chuo cha makardinali, anasimamia msiba wa Papa.

April 19 2005: Ratzinger anachaguliwa kuwa Papa wa 265, katika mkutano wa siri ambao ulifanyika haraka kuliko yoyote iliyowahi kufanyika, siku 5 baadae, yaani Aprili 24, 2005, anasimikwa rasmi mbele ya umma.

Agosti 18-21, 2005: Afanya safari yake ya kwanza, atoka kwenda siku ya vijana duniani, Cologne, Ujerumani. Septemba 24, 2005: akutana na mwanazuoni mpinzani wa utawala katika makazi yake ya kipindi cha kiangazi, na Disemba 25, 2005: Akasaini waraka wa kwanza kwa viongozi wa makanisa, ujumbe ukisema, "Mungu nu Pendo", na ukasambazwa Januari 25, 2006.

Mei 28, 2006: Katika safari yake Poland, kambi ya Auschwitz, kambi mojawapo zilizokuwa za kutesea mateka wa kivita, hasahasa Wayahudi. Na Septemba 12, 2006: wakati anatembelea Ujerumani, akatoa hotuba katika chuo kikuu cha cha Regensburg ambapo ilizua hasira kwa Waislamu, kwa kunukuu kiongozi mmoja wa Byzantine, ambaye alihusisha mafundisho ya Mtume Muhammad kama uovu na kinyume na ubinadamu, hasahasa "amri yake ya kuezeza kwa upanga imani"

Aprili 16, 2007: Toleo la kwanza la "Yesu wa Nazarethi" lakamilika kwenye sherehe yake ya kuzaliwa ya umri wa miaka 80. Kikatolewa Aprili 13, na ilipofika Mei 27, 2007 akasaini barua kwa Kanisa Katoliki nchin China, akiwataka kuungana chini ya mamlaka yake, ikachapwa Juni 30.

Julai 7, 2007: Akaondoa vizingiti katika kusheherekea siku ya Umma ya Latin. Aprili 20, 2008: katika safari yake nchini Marekani, akawaombea wahanga wa shambulio la ugaidi la Septemba 11, 2001.

Julai 19, 2008: Wakati akiwa safarini Australia, kwa ajili ya siku ya vijana duniani, akakutana na wahanga walioingiliwa kimaumbile na viongozi wa kidini, na akawaomba msamaha kwa kutaabika kwao. Januari 21, 2009: akaongeza adhabu ya kuwatenga maaskofu wanaopinga kuwa kulikuwa na mateso kwa wakristo na Wayahudi kutoka kwa askari wa utawala wa Hitler. Maaskofu hawa ni Richard Williamson na wengine watatu. Lakini Januari 24, akaondoa adhabu yake.

Machi 10, 2009: Akubali makosa ya kwenye suala la Williamson, na kusema kuwa ni lazima Vatican watumie vizuri vyombo vya mitandao ili kuepusha utata kwenye jamii. Barua ikatolewa Machi 12 - Machi 17, 2009 akiwa njiani kwenda Cameroon, akawaambia waandishi waliokuwepo kwenye ndege, kuwa kondom sio suluhisho la UKIMWI, na kwamba linaweza kuleta madhara zaidi, jambo ambalo likazua kukosolewa.

Mei 11, 2009: Akitembelea Mji Mtakatifu, akaweka taji la maua kwenye kumbukumbu ya Yad Vashem, na kusema kuwa wahanga wa mauaji ya halaiki "wamepoteza maisha yao, lakini hawatopoteza majina yao kamwe." 

Juni 29, 2009: waraka wa tatu kwa viongozi wa dini wasainiwa, "Sadaka katika Kweli", na kutolewa Julai 7, 2009.

Julai 17, 2009: Akavunjika mkono wa kuume alipoanguka usiku kwenye nyumba yake ya kipindi cha kiangazi.
Okotba 20, 2009: Vatican yatangaza kuwa Papa amerahisisha kwa Waanglikana kubadili na kujiunga na Katoliki.
Machi 19, 2010: Akawashukia maaskofu wa Ireland kwa kushindwa kutoa hukumu nzuri katika kesi iliyohusu unyanyasaji kwa watoto, bila kueleza majukumu ya Vatican kwenye suala hilo katika barua iliyotlewa Machi 20.
Mei 1, 2010: Aamuru mabadiliko makubwa ndani ya Jeshi la Kristo baada ya kubaini kuna ubadhilifu kwa aliyeanzisha
Septemba 16-19, 2010: Karika safari yake ya kwanza ya kitaifa kuitembelea Uingereza, akutana na Malkia Elizabeth II, Askofu Mkuu wa Canterbury, Rowan Williams na kutangaza utakatifu kwa John Henry Newman wa Anglikan.

je? unafahamu huyu??????????????????

MAKALA: SIPHO MAKHABANE GWIJI LA MZIKI ALIYETANGAZA KUSTAAFU

Sipho Makhabane. ©Iol.co.za
Sipho Makhabane si jina geni katika tasnia ya muziki wa injili barani Africa ukifananisha na majina ya wanamuziki wengine kama Joyous Celebration ama Sfiso Ncwane, yeye ni mmoja wa magwiji wa uimbaji nchini kwake Afrika ya kusini akiwa ameshiriki katika shughuli mbalimbali za kiroho na kijamii mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 45

Gwiji hili la muziki ambalo lilitangaza kustaafu uimbaji mnamo mwaka 2010 ingawa mwaka jana alitoa album nyingine mpya akiwa ana miliki kampuni kubwa inayotoa wanamuziki wapya kila kukicha ya "Big Fish" aliacha shule akiwa darasa la tano kutokana na ugumu wa maisha na kuamua kufanya kazi katika shamba la miwa la Kaaruls huko Mpumalanga(kama ilivyokuwa kwa Rebecca Malope) alifanya hivyo ili kuweza kuwasaidia ndugu zake na mama yake ambao walikuwa wakimtegemea yeye.
Alipotimiza umri wa miaka 17 akahamia kwenye kazi za ujenzi kwenye mbugaa ya Kruger National Park ambako alishiriki katika ujenzi wa nyumba kambini hapo.Akiwa na miaka 21 alikuwa tayari na ujuzi wa kutosha katika kazi ya ujenzi ambapo akapata kazi huko Pienaar kabla hajapata ofa nzuri katika kampuni ya Telkom mnamo mwakaa 1986 kama fundi muda wote huo alikuwa akipenda sana muziki wa injili lakini pia ndio ulikuwa mwanzo wake katika biashara na kujua kwamba atatengeneza pesa nyingi katika muziki.

Akiwa na miaka 25 alifunga ndoa na mkewe ambaye kwa wakati huo alikuwa na miaka 18 hiyo ilikuwa mwaka 1990 na kuanza shughuli yua kununua na kuuza kazi za muziki ndani na nje ya nchi yake. Lakini kwa wakati huo akifanya kazi katika kampuni ya Telkom hamu ya moyo wake ilikuwa ni kurekodi album yake binafsi na kufanikiwa kufanya hivyo na kuonyesha kabisa kupenda kazi ya uimbaji kuliko kuweka sawa mitambo ya simu,lakini ilikuwa shida kuwavutia wasambazaji ambao alitaka wawe wananunua kazi kutoka kwake huku wakiwa hawaamini kama anauwezo huo wa uimbaji mpaka pale waliposikia kazi yake katika moja ya radio maarufu nchini humo ya Swazi a.k.a Ligwalagwala FM huku wimbo uliomtambulisha ulikuwa ni ''Ngitinikela Kuwe''. Ambapo mwaka 1996 gwiji hilo likaamua kuingia mazima kwenye tasnia ya muziki wa gospel na kuachana na kazi yake kwenye kampuni ya simu.




Mwaka 1996 aliachia album iitwayo "Yek'intokozo" wimbo ambao mpaka leo ulioacha alama kwa mashabiki wake kwa kumtambua vyema kupitia wimbo huo, lakini wakati huo tayari alishatoa album nyingine mbili miaka ya 1993 hadi 1999 zikiitwa "THUM'UMLOLO" na "JESU ULIQHAWE". Mwaka 1998 kupitia kampuni ya CCP Records aliachia album yake ya nne iitwayo "Uyigugu" iliyofanya vyema, mwaka 1999 akaachia album iitwayo "Makadunyiswe" moja ya album ambyo GK inaipenda sana. Mwaka 2001 akaachia album ya Calvary ambayo iliuza kufikia kiwango cha unit 21. Mwaka 2002 akaachiwa ''Akukhalwa"iliyokuwa kama album yake ya "Yek'intokozo" ambapo iliuza zaidi ya nakala 70,000, mwaka 2003 akaachia album ya ''Moya wami" ambayo pia iliuza zaidi ya nakala 70,000.

Sipho Makhbane ameshirikiana katika album na waimbaji wakongwe wa nchini kwake kama Jabu Hlongwane, Marehemu Vuyo Mokoena, Lundi, Hlengiwe Mhlaba na wengine wengi pia akiwa nyuma ya mafanikio ya waimbaji lukuki kama Hlengiwe Mhlaba, Ncandweni Christ Ambassadors, Shongwe na Khuphuka Saved Group, na pia akiwa mtayarishaji wa album za waimbaji wengi. Mwaka 2004 aliachia album ya "Nkosi nghibheke" ambayo ilikuwa na vigumu kwa mashabiki wake kuchagua nyimbo zilizomo kwakuwa zote zilikuwa nzuri sana bila kusahau kibao cha "guyizolo" ambacho kilikuwa cha shukrani kwa Mungu ambaye huwa anamtumaini kwa kila kitu, pia aliamua kutoa album ya muziki tupu au ala kupitia album hiyo.
Mwaka 2005 aliachia album chini ya kampuni ya SONY/BMG iitwayo "Umuzi Omuhle" akimshirikisha mwanamama Hlengiwe Mhlaba ikimtambulisha kimataifa zaidi,  kama haikutosha aliachia album yake ya 15 ''Ngiyamemeza" ikiwa ni album yake ya tatu kutoa chini ya SONY/BMG bila kusahau nyimbo alizokuwa akizitoa kila wakati wa pasaka na kubariki watu wengi huku kampuni yake ikiwa ni moja ya kampuni kubwa kabisa nchini Afrika ya kusini. Amewahi kuimba jukwaa moja na waimbaji kama Kirk Franklin akipata tuzo mbalimbali kama SAMA, Crown, na nyinginezo ikiwemo kutajwa kwenye tuzo za Kora ambazo zilikuwa maarufu barani Afrika.

TUJITAHIDI KUONEKANA TUMEKUBALIWA NA MUNGU TUSIKATE TAMAA


PICHA ZA GRADURATION YA FORM SIX  MWEMBETOGWA ZA RUTH MASSABA

MSHUKURU MUNGU KWA KUKUWEZESHA KUFIKIA HAPO SEMA ASANTE


wazazi  wa  ruth pamoja na majirani zao katika picha ya pamoja


Ruth mashaba katika pozi

denis nyali mtangazaji wa overcomers radio akikabidhi zawadi kwa ruth

HONGERA RUTH SAMWELI MASHABA








 Siku ya ijumaa ya tare 1.2.2013 familia ya mchungaji samweli masaba wa kanisa la aict mkoani iringa
walikuwa na furaha kubwa kutoka kwa binti yao ruth masaba ambaye alihitimu kitado cha sita kutoka shele ya sekondari ya mwembetogwa iliyopo mkoani iringa

YUPO HAPA YA LISU KUZINDULIWA LEO JIJI DAR

mwimbaji wa nimbo za injili john lisu akiwa uweponi
                        Alive is jehover leo kwa wakazi wa dar moto lazima uatawaka

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog