Home » » je? unafahamu huyu??????????????????

je? unafahamu huyu??????????????????

MAKALA: SIPHO MAKHABANE GWIJI LA MZIKI ALIYETANGAZA KUSTAAFU

Sipho Makhabane. ©Iol.co.za
Sipho Makhabane si jina geni katika tasnia ya muziki wa injili barani Africa ukifananisha na majina ya wanamuziki wengine kama Joyous Celebration ama Sfiso Ncwane, yeye ni mmoja wa magwiji wa uimbaji nchini kwake Afrika ya kusini akiwa ameshiriki katika shughuli mbalimbali za kiroho na kijamii mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 45

Gwiji hili la muziki ambalo lilitangaza kustaafu uimbaji mnamo mwaka 2010 ingawa mwaka jana alitoa album nyingine mpya akiwa ana miliki kampuni kubwa inayotoa wanamuziki wapya kila kukicha ya "Big Fish" aliacha shule akiwa darasa la tano kutokana na ugumu wa maisha na kuamua kufanya kazi katika shamba la miwa la Kaaruls huko Mpumalanga(kama ilivyokuwa kwa Rebecca Malope) alifanya hivyo ili kuweza kuwasaidia ndugu zake na mama yake ambao walikuwa wakimtegemea yeye.
Alipotimiza umri wa miaka 17 akahamia kwenye kazi za ujenzi kwenye mbugaa ya Kruger National Park ambako alishiriki katika ujenzi wa nyumba kambini hapo.Akiwa na miaka 21 alikuwa tayari na ujuzi wa kutosha katika kazi ya ujenzi ambapo akapata kazi huko Pienaar kabla hajapata ofa nzuri katika kampuni ya Telkom mnamo mwakaa 1986 kama fundi muda wote huo alikuwa akipenda sana muziki wa injili lakini pia ndio ulikuwa mwanzo wake katika biashara na kujua kwamba atatengeneza pesa nyingi katika muziki.

Akiwa na miaka 25 alifunga ndoa na mkewe ambaye kwa wakati huo alikuwa na miaka 18 hiyo ilikuwa mwaka 1990 na kuanza shughuli yua kununua na kuuza kazi za muziki ndani na nje ya nchi yake. Lakini kwa wakati huo akifanya kazi katika kampuni ya Telkom hamu ya moyo wake ilikuwa ni kurekodi album yake binafsi na kufanikiwa kufanya hivyo na kuonyesha kabisa kupenda kazi ya uimbaji kuliko kuweka sawa mitambo ya simu,lakini ilikuwa shida kuwavutia wasambazaji ambao alitaka wawe wananunua kazi kutoka kwake huku wakiwa hawaamini kama anauwezo huo wa uimbaji mpaka pale waliposikia kazi yake katika moja ya radio maarufu nchini humo ya Swazi a.k.a Ligwalagwala FM huku wimbo uliomtambulisha ulikuwa ni ''Ngitinikela Kuwe''. Ambapo mwaka 1996 gwiji hilo likaamua kuingia mazima kwenye tasnia ya muziki wa gospel na kuachana na kazi yake kwenye kampuni ya simu.




Mwaka 1996 aliachia album iitwayo "Yek'intokozo" wimbo ambao mpaka leo ulioacha alama kwa mashabiki wake kwa kumtambua vyema kupitia wimbo huo, lakini wakati huo tayari alishatoa album nyingine mbili miaka ya 1993 hadi 1999 zikiitwa "THUM'UMLOLO" na "JESU ULIQHAWE". Mwaka 1998 kupitia kampuni ya CCP Records aliachia album yake ya nne iitwayo "Uyigugu" iliyofanya vyema, mwaka 1999 akaachia album iitwayo "Makadunyiswe" moja ya album ambyo GK inaipenda sana. Mwaka 2001 akaachia album ya Calvary ambayo iliuza kufikia kiwango cha unit 21. Mwaka 2002 akaachiwa ''Akukhalwa"iliyokuwa kama album yake ya "Yek'intokozo" ambapo iliuza zaidi ya nakala 70,000, mwaka 2003 akaachia album ya ''Moya wami" ambayo pia iliuza zaidi ya nakala 70,000.

Sipho Makhbane ameshirikiana katika album na waimbaji wakongwe wa nchini kwake kama Jabu Hlongwane, Marehemu Vuyo Mokoena, Lundi, Hlengiwe Mhlaba na wengine wengi pia akiwa nyuma ya mafanikio ya waimbaji lukuki kama Hlengiwe Mhlaba, Ncandweni Christ Ambassadors, Shongwe na Khuphuka Saved Group, na pia akiwa mtayarishaji wa album za waimbaji wengi. Mwaka 2004 aliachia album ya "Nkosi nghibheke" ambayo ilikuwa na vigumu kwa mashabiki wake kuchagua nyimbo zilizomo kwakuwa zote zilikuwa nzuri sana bila kusahau kibao cha "guyizolo" ambacho kilikuwa cha shukrani kwa Mungu ambaye huwa anamtumaini kwa kila kitu, pia aliamua kutoa album ya muziki tupu au ala kupitia album hiyo.
Mwaka 2005 aliachia album chini ya kampuni ya SONY/BMG iitwayo "Umuzi Omuhle" akimshirikisha mwanamama Hlengiwe Mhlaba ikimtambulisha kimataifa zaidi,  kama haikutosha aliachia album yake ya 15 ''Ngiyamemeza" ikiwa ni album yake ya tatu kutoa chini ya SONY/BMG bila kusahau nyimbo alizokuwa akizitoa kila wakati wa pasaka na kubariki watu wengi huku kampuni yake ikiwa ni moja ya kampuni kubwa kabisa nchini Afrika ya kusini. Amewahi kuimba jukwaa moja na waimbaji kama Kirk Franklin akipata tuzo mbalimbali kama SAMA, Crown, na nyinginezo ikiwemo kutajwa kwenye tuzo za Kora ambazo zilikuwa maarufu barani Afrika.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog