Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Tarehe 26 Juni 2015















Magereza yaaswa kuruhusu wafungwa kujiandikisha bvr.


JESHI la Magereza nchini limeshauriwa kuhakikisha wanaruhusu wafungwa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo wa kielektroniki (BVR), unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Hatua hiyo ni kuwawezesha kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi katika uchaguzi ujao.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mratibu wa marafiki wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Noel Nnko wakati walipotembelea Gereza la Wilaya ya Same na kutoa misaada mbalimbali kwa wafungwa ikiwemo utoaji wa elimu ya kujiandikisha.

Nnko alisema licha ya kutolewa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura makundi mbalimbali katika jamii yamekuwa yakisahaulika ikiwemo wafungwa waliopo magerezani katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo ni vema viongozi wa Jeshi la Magereza nchi wakatupia macho suala hilo kwa kuhakikisha wafungwa wanaoruhusiwa kujiandikisha katika daftari hilo wanapata haki hiyo kwa mujibu wa sheria.

“Tumepitia sheria tumejiridhisha kuwa wafungwa wasioruhusiwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kupiga kura ni wafungwa waliohukumiwa vifungo vya maisha na kifo.

“Hivyo natoa rai yangu kwa viongozi wa magereza kutenda haki kwa wafungwa wengine kwani kundi hili limekuwa halipewi kipaumbele katika masuala mbalimbali ya kijamii,” alisema Nnko.

Katika hatua nyingine, Nnko aliwataka wafungwa hao kuacha tabia ya kushabikia viongozi wa kisiasa bali kujiandikisha katika daftari hilo hatua ambayo itawawezesha kupata viongozi bora kwa ustawi wa taifa kwa ujumla.

Akina Mama Waandamana Kudai miili ya Waliouawa na Askari Kwa Kupigwa Risasi Mkoani Simiyu


KINAMAMA kutoka Kata ya Bukundi Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, wameandamana hadi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Erasto Sima, kushinikiza wapewe miili ya vijana wao wawili waliouawa na askari Mei 29, mwaka huu.
 
Vijana hao Gineu Gidahasi na Gitienga Gidahasi ambao ni ndugu wa familia moja wanadaiwa kupigwa risasi na askari wa Kampuni ya ulinzi ya Mwiba Holding kwa madai ya kuingiza mifugo eneo pori la makao ambalo kampuni hiyo imewekeza.
 
Kinamama hao walifika katika ofisi ya Mkuu huyo wa wilaya saa mbili juzi asubuhi  ambapo walilalamikia kitendo cha vijana wao kuuawa na kisha miili yao kutoonekana na kumwomba Sima kuagiza kupatiwa miili hiyo ili waweze kuifanyia mazishi na iwapo itashindikana watakwenda kwa Rais Jakaya Kikwete kuomba msaada huo.

“Tumechoka na manyanyaso kutoka kwa mwekezaji huyu, kilichotuleta hapa tunahitaji tupatiwe miili ya vijana wetu tukaifanyie mazishi kwa heshima zote za kabila letu na iwapo utashindwa kufanya hivyo basi tutakwenda Ikulu tumuombe Rais Kikwete atusaidie,” alisema Udamulela Gitasori  mkazi wa kijiji cha Lukale.

Walisema hadi sasa zaidi ya vijana sita wameuawa tangu mwaka 2013 kwa madai ya kuingiza mifugo katika eneo la pori hilo ambalo linapakana na vijiji vya Mwabagimu, Lukale na Bukundi na hivyo wamekuwa wakiishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao.

Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Meshack Opulukwa (Chadema), aliitupia lawama serikali kwa kushindwa kulipatia ufumbuzi suala la wafugaji kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa mwekezaji huyo licha ya kupatiwa taarifa na hivyo alimwomba Sima kusitisha shughuli zinazofanywa na Mwiba hadi hapo miili hiyo itakapopatikana.

Akijibu malalamiko hayo kwa kifupi Sima alisema serikali wilayani humo imeshaanza kulishughulikia suala hilo na tayari wote waliohusika na mauaji hayo wameshakamatwa.

Lowassa Avunja Rekodi Mkoani Shinyanga.......Wananchi Waumizana Wakigombea Kumuona, Avuna Wadhamini 7,114


Mh. Lowassa, akipokea fomu zilizojazwa na wana CCM waliomdhamini mkoani Shinyanga, kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Shin yanga mjini Charles Sangula, Juni 11, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipungia mkono wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, alipokuwa akiondoka ofisi za chama hicho wilaya ya Shinyanga mjini mara baada ya kupata wana CCM wa kumdhamini .
 
Mh. Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, jana  amevunja rekodi ya kupata wadhamini 7,114, idadi  ambayo  ni kubwa kuliko  mgombea  mwingine  yeyete  ndani  ya  CCM hadi sasa. 

Furaha ya kumuona Mh. Lowassa, ilitawala ukumbi mzima
Wana CCM waliofika kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, wakishangilia wakati akiingia ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga, wakisukumana ili wapate kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015, ili kuomba wanachama wenzake wa chama hicho wamdhamini.

Wakazi Wa Mgao Wamvaa Halima Mdee Kwa Kuwadhalilisha......Wamtaka Afute Kauli Yake


KUFUATIA taarifa iliyotolewa  na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kuhusu utoaji wa ardhi kwa bilionea Alhaji Aliko Dangote, wakazi wa kijiji cha Mgao, Halmashauri ya Mtwara Vijijini wamemtaka kufuta kauli yake.

Wakitoa malalamiko yao kwa vyombo vya habari, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho ambao walijitambulisha kwa majina ya Seif Said na Mohamed Njiti, walisema kuwa kitendo cha ardhi yao kulinganishwa na kaniki na kipande cha kanga kimewasikitisha.

Walisema uthamini wa ardhi umeshaanza, wanatarajia kulipwa Sh milioni 10 kwa ekari moja, huku wakipata malipo ya mimea iliyopo kwenye mashamba yao, zoezi ambalo bado linaendelea katika maeneo ya vijiji vya Kisiwa na Mgao.

Kwa upade wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abdulahman Shaha, alisema amesikitishwa na taarifa iliyotolewa kwa kulinganisha ardhi yao na kipande cha kaniki.

“Ile kauli sio sahihi, ilibidi aje Mgao apate taarifa sahihi ili akatoe bungeni, sisi tuko katika tathmini ya ardhi, kila mwananchi atalipwa stahiki yake,  walipaji wa ardhi hii ni Mamlaka ya Bandari Tanzania siyo Dangote,”  alisema Shaha. 

Naye Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Mtwara, Hebel Mwasenga, alisema mamlaka hiyo inamiliki eneo la hekta 1,000, ambapo mwekezaji huyo amepewa eneo la hekta 25 kwa ajili ya ujenzi wa bandari ndogo.

Mwanamke Atiwa Mbaroni Akituhumiwa Kumuua Mwanae Mchanga Kwa Kumtumbukiza Chooni


JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Dainees Fredrick (30), mkazi wa Kambi ya Raha, wilayani Hai, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mchanga muda mfupi baada ya kumzaa kwa kumtumbukiza chooni.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho siku moja baada ya kujifungua ambapo alimfunga mtoto huyo wa kiume kwenye kanga na kumweka kwenye mfuko wa plastiki kisha kumtumbukiza chooni.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, katika taarifa yake alisema tukio hilo lilitokea Juni 10, saa tatu usiku, Mtaa wa Kambi ya Raha, ambapo waliofanikisha kukamatwa kwake ni majirani anaoishi nao.

Alisema Rose Komely alisikia sauti ya kichanga kikilia ndani ya choo baada ya kwenda kujisaidia, ndipo alipowaeleza wapangaji wengine na kwenda chumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumkuta akiwa amekaa huku akiwa hana ujauzito analalamika maumivu ya tumbo.

Ngonyani alisema kuwa mtoa taarifa alimuacha mtuhumiwa akiwa na mwenzake kisha kutoa taarifa kwa balozi Editha John ambaye alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Hata hivyo, licha ya Jeshi la Polisi kufanikiwa kufika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumtoa mtoto katika choo alichokuwa ametupwa tayari mtoto alikuwa amekufa.

Mtuhumiwa wa tukio hilo la mauaji ya kichanga anashikiliwa na Polisi na kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Hai, huku akiwa chini ya ulinzi akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.

Kortini kwa Kulawiti Mtoto


MKAZI wa Mbezi Beach   Dar es Salaam, Tuntutye Mwasyete (25), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumlawiti mtoto (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa mwaka mmoja.
 
Mbele ya Hakimu, Lilian Rutehangwa, Wakili wa Serikali Masini Musa alidai   kwamba tukio hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu  huko Kawe.
 
Mtuhumiwa alikana shtaka hilo na  alirejeshwa mahabusu   hadi Juni 24 mwaka huu yatakaposomwa  maelezo ya awali

MIAKA HAMSINI YA UHURU WAKAZI WA VIWENGI IRINGA WALIA NA MAJI


Hawa ni wananchi wa kijiji cha lundamatwe kitongoji cha viwengi jimbo la kilolo mkoani iringa nyambizi la sunrise power nuru fm 93.5 iringa, Limewatembelea na kuzungumza nao wananchi hawa hakika wanashida nyingi ikiwemo maji ni tatizo kubwa,
Kama unavyoona picha hayo ndio maji wanayokunywa na kuoga na matumizi yote licha ya kuwa ni machafu bado maji haya huisha mapema. na kujikuta wakitumia muda mwingi kutafuta maji.
Jadili pamoja nami kupitia ukurasa huu au kupitia matangazo ya Radio Nuru Fm 93.5 iringa kesho asubuhi saa 12:30 - 4 kamili.
Wananchi hawa wana viongozi kama.....
1. diwani
2. mtendaji.
3. mwenyekiti.
4. mbunge
5. mkurugenzi
6. mkuu wa wilaya.
7. mkuu wa mkoa.
8. waziri.
9. waziri mkuu
10. Rais.
11. na wengine wengi katika idara zilizopo...

Nani kashindwa kutimiza wajibu wake ili kuwasaidia wananchi hawa kati ya hao hapo juu?

MAGUFULI AENDELEA KUSAKA WADHAMINI....ISHU IKAWA KUZUNGUMZIA!!

 
Waziri wa ujenzi Dkt. John Pombe Magufuri ambaye pia ni miongoni mwa wagombea waliochukua fomu za kuwania mbio za uraisi wa awamu ya tano amesema hawezi kuthubutu kuzungumza chochote mbele ya hadhara ya wananchi katika kipindi hiki kigumu cha kutafuta wadhamini na kwamba kufanya hivyo nikukiuka maadili ya chama chake.

June 10 2015.. Hizi ndio stori kubwa za #Magazeti 17 ya Tanzania leo>> Udaku,Michezo, Dini na Hardnews

DSC03523

DSC03522 DSC03523 DSC03524 DSC03525 DSC03526 DSC03527 DSC03528 DSC03529 DSC03530 DSC03531 DSC03532 DSC03533 DSC03534 DSC03535 DSC03536 DSC03537 DSC03538 DSC03539 DSC03540 DSC03541 DSC03542 DSC03543 DSC03544 DSC03545 DSC03546 DSC03547 DSC03548 DSC03549 DSC03550 DSC03551 DSC03552 DSC03553 DSC03554 DSC03555

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog