UKATILI WA KUTISHA TIZAMA HABARI UJIONEE INASIKITISHA SANA

DAS JOSEPH CHINTIKA: ISMANI HAKUNA NJAA

 Katibu tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintika akizungumza na waandishi wa habari ofisni kwake.

 
Na Fredy Mgunda,Iringa

KATIBU tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintika amesema kuwa tarafa ya ismani haina njaa kama ambavyo maneno yanayozagaa mitaani kuwa ukanda wa ismani kuwa kuna njaa.
Akizungumza na blog hii Chintika alisema kuwa kumekuwa na wanasiasa wanaoeneza kuwa tarafa ya ismani kuna njaa wakati hali halisi sio hiyo na kuongeza kuwa eneo hilo linachakula cha kutosha na hakuna tatizo la njaa.
“Angalia mvua zinanyesha kwa wingi na wananchi wamelima kwa wingi na mazao yanakuwa vizuri hivyo ismani hakuna njaa na sijapokea taarifa yoyote ile ya kuwepo kwa njaa kwa kuwa nimekuwa nikifanya ziara katika maeneo hayo mara kwa mara na nimejihakikishia kuwa hakuina njaa hali ya chakula ni nzuri na kuwaomba wananchi kuacha kuwasikiliza wanasiasa”.alisema Chintika
Chintika aliwataka wananchi kuacha kutumia mazao ya mahindi,mtama na uwele kupikia pombe kwa kuwa kufanya hivyo kutapunguza uwepo wa chakula katika eneo hilo.
Unakuta mtu anashawishiwa kuuza mahindi kwa mpika pombe wakatyi anajua kuwa hana chakula cha kutosha nasema ni marufuku kwa wananchi kupika pombe kwa kutumia mahindi,uwele na mtama ili  kuendelea kutunza chakula hicho.
Aidha Chintika alisema kuwa sasa ni fursa kwa wafanyabiasha kuuza mahindi katika maeneo mbalimba ya wilaya ya iringa kwa kuwa bei ya mahindi kwa sasa ni nzuri.
Hivi hawa wanansiasa wanayatoa wapi maneno ya uongo kuwa ismani kuna njaa naomba waje na takwimu na sio kuposha wananchi serikali ndio inaweza kutangaza kama sehemu kuna njaa na sio mtu mwingine yoyote.
“Serikali ndio chombo cha mwisho kuthibitisha kuwa ismani kuna njaa sio kila mtu anaweza kuongelea mambo ya serikali naomba hawa wanansiasa waache mara moja kupotosha wananchi na wakiendelea kupotosha jamii tutawachukulia hatua za kisheria maana hatuna tatizo la chakula katika tarafa ya ismani”.alisema Chintika
AUAWA KWA KUTENGANISHWA SHINGO NA KIWILIWILI NA KUTOMEA NA KICHWA KUSIKOJULIKANA
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo
Na Fredy Mgunda,Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya iringa kuacha tabia ya kuamini na kujihusisha na maswala ya imani za kishikina pamoja na kujichukulia hatua mikononi.
Ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mikong’wi kata ya kihologota wilaya ya iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na kutelekeza kiliwili chake.
“Kwanini watu wajichukulie hatua mkononi wakati serikali,jeshi la polisi,mahakama,makanisa na misikiti huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote  na haya mambo ya kishikina serikali haiamini da nasikitika sana kwa tukio la leo ni baya sana”alisema Kasesela
Kasesela alisema kama wilaya wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.
“Wilaya ya Iringa ilikuwa imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa keli lazima jeshi la polisi lifanye uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha mikong’wi na lazima tukomeshe na kuwa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela 
Kasesela ameeleza kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni hasani nyalusi mkazi wa kijiji cha mikong’wi tarafa ya Isman mkoani Iringa.
Aidha Kasesela amewaomba viongozi wa dili mbalimbali kutoa elimu ya mungu na kukemea maswala ya kishikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji cha Mikong’wi Majorino Muyinga Anaeleza kuwa Mnamo tarehe 06/04/2017 huko kitongoji cha Utitiri kijiji cha Mikong’wi kata ya Kihorogota tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa vijijini Mkoani Iringa alisema kuwa Hassan Nyalusi alikutwa akiwa ameuawa nje ya nyumba yake na mtu/watu wasiofahamika na mwili ukiwa hauna kichwa na uchunguzi wa daktari umefanyika na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehehemu kwa taratibu za mazishi laiki mtu mmoja Jackson Nyalusi anashikiliwa na polisi kuhusishwa na mauaji haya,bado upelelezi unaendelea
 

Magazeti ya Leo tare 5 jumatano soma hapa



Kumbe hata wabunge walikumic Jk


Mkutano wa saba wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo Dodoma. Mkutano huu ni kwa ajili kupitisha bajeti ya Serikali itakayowasilishwa bungeni June 15 mwaka huu.
Kati ya wageni waliotambulishwa leo mbungeni ni pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete,

http://www.malunde.com/2017/04/majambazi-watatu-waliovaa-hijabu-wauawa.html

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi  wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kukaidi amri ya kutakiwa kusimama eneo la kizuizi cha Mwembe Muhoro wilayani Rufiji, mkoani Pwani.

Watu hao walikuwa wamepakiana kwenye pikipiki moja huku wakiwa wamevaa hijabu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pikipiki nyingine mbili zilifanikiwa kukimbia.

Akielezea juu ya tukio hilo alifafanua,lilitokea Aprili 2 mwaka huu majira ya mchana ,Muhoro ,Rufiji barabara kuu ya Dar es Salaam Lindi.

“Siku ya tukio askari walipata taarifa kuwa kulikuwa na pikipiki tatu zikitokea Kibiti kwenda mikoa ya Kusini zikiwa zimebeba watu watatu kila moja “

“Miongoni mwa pikipiki hizo kati yake mbili wamebebwa watu waliovaa hijabu,” alisema Lyanga.

Alisema askari wa barabarani walipewa taarifa katika kizuizi cha Mparange na kuwasimamisha ili wawahoji lakini walikataa na kupita ambapo waliwajulisha wenzao kwenye kizuizi cha Ikwiriri lakini walikaidi kusimama.

“Baada ya hapo walifika kizuizi cha Ikwiriri lakini bado walikaidi kusimama na kuendelea kukimbia ndipo walipofika kituo cha Muhoro “

“Hata hivyo hawakusimama na askari waliokuwa doria wakiwa kwenye gari waliwafuatilia na wakavuka daraja la Mkapa na waliwapa onyo kwa kupiga risasi hewani,” alisema Lyanga.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog