JIANDAE KWA TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU


              Alex msama akielezea mpango mkakati wa maandalizi ya tamasha





Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu Tamasha la kila mwaka la Pasaka, Alex Msama, amesema tukio hilo linalohusisha onyesho la muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya nchi, ni la kila mtu kwani litaendelea kusaidia makundi mbalimbali yasiyojiweza na walemavu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msama alisema ingawa wao ni waratibu, lakini lengo hasa la tamasha hilo ni kupata kiasi cha fedha za kuwapatia watu wanaohitaji msaada, kama vile watoto yatima, walemavu wa aina mbalimbali na wale wanaokumbwa na majanga makubwa.
“Hili ni tamasha lao, wao ndiyo wadau wakubwa kwa sababu wananufaika nalo. Kila mtu ni shahidi kuwa tumekuwa tukitoa misaada ya aina mbalimbali kwa makundi maalum ya watu.

Hata hivyo, ni vyema pia tukaweka wazi kuwa wanaowezesha haya yote ni watu wanaokuja kuunga mkono tukio hili linalofanyika kila mwaka,” alisema Msama.

Kuhusu tamasha la mwaka huu, Msama alisema hawezi kulizungumzia kwa undani kwa sasa kwa vile bado wanaendelea na taratibu za kupata kibali chake na wakishafanikisha suala hilo, wataweka wazi kwa umma ili ujue.

Katika tamasha la mwaka jana lililofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, waimbaji mbalimbali maarufu walipanda jukwaani na kutoa burudani safi.

JE? UNAMFAHAMU MUNGU ALIKO MTOA HUYU???????????

                                            john shabani akiwa katika pozi
                              




John S. Shabani ni mzaliwa wa kijiji cha Kirando katika kitongoji cha Nyankima, kata ya sunuka, Wilaya ya Kigoma Vijijini, Nchini Tanzania. Ukoo wake ni waumini wazuri wa dini ya kiislam (Islamic Religion).

Baada ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi kirando, alijiunga na elimu ya sekondari, lakini kutokana na itikadi za kidini, alijikuta akiwa katika wakati mgumu wa kupigwa vita na wazazi, ni baada ya uamuzi wake wa kujiunga na Dini ya kikristo. Hivyo John ameishi miaka mingi akiwa mbali na wazazi wake, lakini hata hivyo hakukata tamaa.

Mwaka 1992, John akiwa kijana mdogo, alipata ufadhili wa kwenda nchni Kongo (Zamani Zaire), ambako huko alijifunza muziki na kusoma Chuo cha Biblia (Bible knowledge), na huko kipaji chake cha kutunga nyimbo na kuimba kilijitokeza kwa kasi, hata akatokea kupendwa sana.

John hakutaka kuona mtu yeyote akiwa katika hali ya kukata tamaa, maana alifahamu madhara yake. Kwasababu hiyo, alianzisha vikundi mbalimbali vya vijana akiwa na lengo la kuwaelimisha ili kujikwamua katika hali ya kukata tamaa na kutokujihusisha na vitendo viovu kama madawa ya kulevya, Ukahaba na anasa za kila aina, mambo ambavyo aliyapiga vita sana.

John ameishi miaka mingi kama yatima, lakini hali hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kuwa na tabia njema, kumheshimu na kumthamini kila mtu, mambo yaliyompelekea kupata kibali machoni pa wengi hata kuwa mfano wa kuigwa. Amekuwa msaada kwa Vijana wengi (Ndani na nnje ya nchi) na kuwakwamua wengi waliokuwa wamekata tamaa na kujihusisha na vitendo viovu. Pia kutokana na ujuzi wa muziki alioupata na pia kipaji kikubwa alichonacho cha kutunga, kuandika nyimbo na kuimba, John amekuwa msaada kwa waimbaji mbalimbali binafsi na vikundi ndani na nje ya nchi, hasa nyimbo za Injili. Ni mwalimu bora na mshauri kwa waimbaji. Wengi waliopitia kwake sasa ni waimbaji wazuri na maarufu.

Mwaka 2001 John alifunga pingu za maisha na binti aitwaye Debora Shabani na mwaka 2002 walipata mtoto wa kike. Alimwita mwanaye Joyce, akiwa na maana ya kuyasahau maisha ya huzuni na shida na kujitabiria maisha ya furaha.

Mwaka 2004, John aliajiriwa katika kampuni ya Msama promotions ya jijini Dare es salaam, kampuni inayojihusisha na kuinua vipaji na pia kuwainua vijana na watu wa rika na jinsia zote waliokata tamaa ya maisha n.k, na hasa wale walioko vijiweni wakijihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba n.k. Kampuni hiyo imewasaidia Vijana wengi na Jamii kwa ujumla, na wengi wamejikomboa kimaisha

Tarehe 19/03/04, John alirekodi Album yake aliyoiita “Marufuku kukata tamaa
Album ambayo imewasaidia wengi waliokata tamaa na kuwapa matumaini mapya. Album hiyo na nyingine alioirekodi mwaka 2009 inayoitwa “Huu ni wakati wangu”, zimekuwa msaada mkubwa kwa kila aliye au anayezinunua, zimegusa na kuinua mioyo ya watu wengi. Kwani amepokea shuhuda nyingi ndani na nnje, hata za wale waliodiriki kujiua, lakini baada ya kusikiliza nyimbo hizo waliahirisha. “Nakusii nunua kanda hizo, naamini zitakusaidia”. Pia utakuwa mchango wako kwa kutimiza ndoto na malengo ya John.

John ametembelea nchi mbalimbali, akijifunza maisha ya watu. Amegundua kwamba karibu asilimia kubwa ya wanadamu, awe maskini, tajiri, msomi au asiye na elimu, wenye vyeo au waajiriwa, watoto kwa wakubwa, wanaume kwa wanawake, awe mzungu au mweusi n.k, wote kwa njia moja au nyingine wamepitia katika hali ya kukata tamaa au kukatishwa tamaa na jambo fulani, mtu, watu, hali au mazingira fulani. Ndipo mwaka 2006, alipata maono na msukumo mkubwa wa kuandika Kitabu ambacho kitakuwa msaada kwa njia moja au nyingine kwa kila atakayekipata.

Tarehehe 11/7/08 ni siku ambayo John hawezi kuisahau. Siku ya huzuni na majonzi, siku ya kilio na kuomboleza. Ni siku alipofariki mke wake mpendwa na mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili, Debora Shabani, mwimbaji aliyegusa mioyo ya watu wengi ndani na nnje ya nchi, mwimbaji ambaye msiba na mazishi yake yalihudhuriwa na maelfu ya watu, wakiwepo Maaskofu, Wachungaji, Waimbaji binafsi, Kwaya pamoja na viongozi mbalimbali wa serekali. Hata hivyo, John hakukata tamaa.

Tarehe 26.04. 2009, John alitunukiwa tuzo ya heshima pamoja na cheti (certicate of appreciation) kwa kutambua mchango wake kwa ajili ya kuinua vipaji na pia kuchangia kuinua muziki wa Injili Afrika mashariki na kati. Pamoja na hayo amekua akianzisha makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu maisha ya kujitegemea, kujishughulisha na kuhepukana na vitendo viovu kama wizi, ujambazi, utumiaji madaswa ya kulevya, ukahaba n.k. Tuzo hiyo ilitolewa na kampuni moja maarufu Tanzania yenye makao makuu jijini Dar es salaam (Christian promoters Ltd).

John ameanzisha huduma inayoitwa Never give up “Usikate tamaa” Ambayo anategemea kuisajili wakati wowote. Huduma hii, inalenga kuinua vipaji, mipango na mbinu za kuwakwamua vijana au watu kujihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba, utapeli wizi, ujambazi nk, mambo yanayosabisha magonjwa kama vile ukimwi, kufungwa jela au kufa kabla ya wakati, matokeo yake kuacha wototo wengi yatima na wajane nk. Pia kutafuta ufadhili kwa ajili ya kuaendeleza vijana ki-elimu pamoja na kuwawezesha pale inapobidi. Kwa sasa anayo program inayoitwa Touching voice program (Darasa la uhimbaji)
Ni kwa ajili ya kwaya, Band/vikundi na waimbaji binafsi



NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog