Home » » BAHATI BUKUKU AZINDUA KWA KISHINDO, MILIONI 20 ZATOLEWA NA LOWASSA

BAHATI BUKUKU AZINDUA KWA KISHINDO, MILIONI 20 ZATOLEWA NA LOWASSA


"Mtu yeyote anayeiombea amani anaipenda nchi hii. Leo natoa changamoto waimbaji wa nyimbo za injili wahubiri sana amani."

Ni kauli ya Waziri Mkuu aliyepita, ambaye pia ni mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa DVD ya album ya Dunia Haina Huruma, ya kwake Bahati Bukuku, ambayo imehudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba Jumapili hii.
Gospel Kitaa ilikuwepo kna kushuhudia ambapo, pamoja na kuwataka waimbaji wa nyimbo za injili wahubiri amani, Mh. Lowassa pamoja na marafiki zake walichangia kiasi cha shilingi Milioni 20.

Waimbaji kadhaa walimsindikiza Bahati kwenye uzinduzi huo ambao haukuwa na kiingilio, ambapo injili ilihubiriwa kwa njia ya uimbaji na watu kukata kiu na njaa ya kiroho waliyokuwa nayo, mkongwe Jennifer Mgendi,  Bonny Mwaitege, Neema Gasper, Rebecca Magaba (Ebenezer), Emmanuel Mgogo (Msikilize Mungu),  Majestic Singers wa EAGT Singers, Sarah Mvungi, ni sehemu tu ya waimbaji waliokuwepo.

Bahati Bukuku pia alitumia fursa hiyo kufungua Bukuku Entertainment ambayo iko Kariakoo mtaa wa Mhonda jijini Dar es Salaam, ambapo ni kampuni ya usambazaji itakayoshughulika na waimbaji chipukizi tu, na si waliokwisha toka tayari na kujulikana kwenye jamii.
Jennifer Mgendi akihudumu

MC wa shughuli, Silas Mbise akishuhudia mgeni rasmi anavyopungiwa
Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akiwaaga wananchi
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog