Home » »

MAKALA: CECILE KYENGE, TOKA CHINI KWENDA JUU, KUTOKATA TAMAA KWAMTOA

Dakta Cecile Kyenge katika mojawapo ya mikutano. ©Reuters
Nilipokuwa mtoto, na nikakosea kisha mama aniseme, nilitamani anipige tu mambo yaishe – unajua ni namna gani maneno yanachoma. Ndio maana hata kuna utani kwamba mzaramo anaweza kukusema hadi ukafa. Haya yote ndio yananirejesha kwa Cecile Kyenge, mwanamama wa kwanza kuwa waziri mweusi nchini Italia.

Kila nikimtazama mama huyu mzawa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Napata ahueni – ahueni kwamba hata kama watu wakikupiga kwa maneno, bado unaweza kutekeleza yale uliyonuia kufanya bila chembe ya wasiwasi.

Wanaomsema wanatokea kila upande – kuanzia viongozi wenzake, hadi wananchi ambao anawatumikia. Ugumu anaokutana nao, unaweza pia kulinganishwa na ugumu anaoupata mchezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Mario Ballotelli – ambapo amewahi kuzungumzai historia yake ya kukachwa na wazazi wake akiwa mdogo, na kuasiliwa na familia mojawapo ya wataliano kabla hajawa raia na hatimaye kulitumikia taifa lake jipya kupitia timu ya taifa, akisakamwa na maneno lukuki kuanzia ndani hadi nje ya uwanja.

Balotelli bado ni kijana, na kwa utukutu wake, ameshatoa majibu mengi ikiwamo ya mkato na hata kuwa mkali zaidi pale anapochukizwa na hata bosi wake.

Ninachokiona ndani ya huyu mama ndicho kinanivuta hasa kuandika hivi, na tayari ninajifunza kitu kwake. Ni mvumilivu, asiyetetereka (japo inavunja moyo sana) wala kushambulia wale ambao wanamtuhumu kwa mambo mengi kwenye nafasi yake ya uwaziri anayeshughulikia uhamiaji.
Dakta Kyenge ofisini. ©Gregorio Borgia/AP
Matukio;
Makamu wa Rais wa senate nchini humo ameshawahi kunukuliwa kisema kuwa anapenda wanyama, na kila akimuangalia Cecile haoni tofauti na nyani aina ya Orangutan. Kauli hiyo ya kiongozi wa juu ilijibiwa kwa ufupi na Bi Kyenge ya kwamba, kama kiongozi huyo ameshindwa kuitumikia nafasi yake, ni vyema basi akaachia kiti.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog