Home » »

MASANJA MKANDAMIZAJI YUKO MAREKANI KUHUBIRI

Masanja alipokuwa jijini New York alipokwenda kwa mara ya kwanza.
Mungu ameendelea kufungua milango kwa mchekeshaji wa kundi la Original Comedy ambaye pia anafanya kazi za kumuhubiri Mungu kijana Emmanuel Mgaya au mwite kwa jina lake la kazi Masanja Mkandamizaji ambaye kwasasa yupo nchini Marekani kwa huduma ya kimungu ambako amealikwa kwa kazi hiyo ikiwa pamoja na kuzungumza na vijana katika miji mitatu ya California, Minnesota pamoja na Dallas.

Masanja amemshukuru Mungu kwa nafasi anayoipata hasa ikizingatiwa kwamba hii ni
mara yake ya pili ambapo amekiri kuwa Yesu ndiye anafanya yote haya katika maisha yake kwakuwa hajawahi kufikiria kwamba siku moja atakanyaga Marekani maana tangu ameanza kazi ya uchekeshaji hajawahi kufika huko ila alipompokea Yesu anaona milango ikifunguka zaidi na zaidi. Masanja akiwa huko akimaliza kilichompeleka amepanga kurekodi baadhi ya vipande vya vipindi vya Original Comedy ambavyo itakuwa kuwafundisha watanzania na vijana nini watu wa Marekani wanafanya.

Aidha katika mahojiano na Silas Mbise kupitia kipindi cha
Gospel Celebration cha WAPO Radio Fm mda mchache uliopita mwigizaji huyo atakuwa nchini Marekani kwakipindi cha mwezi mmoja amemtaka mtangazaji huyo kuoa maana kuchelewa kwake kunafanya wengine kuchelewa mwe mwe mwe Silas si akajikausha ha ha ha, kijana akaishia kukata simu na kusema wakati wa Bwana ukifika atafanya hivyo. Ila kweli anatuchelewesha kha!
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog