AIBU KUBWA! MUUZA GENGE ACHEZEA KICHAPO KWA KUNASWA NA MKE WA MTU

Aibu kubwa! Muuza genge mmoja kwenye Soko la Mji Mpya mjini hapa ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akichezea kichapo kwa madai ya kunaswa na mke wa mtu kisha kutembezwa mtupu mtaani.

Muuza genge aliyechezea kichapo baada ya kunaswa na mke wa mtu na kutembezwa mtupu mtaani.
Fumanizi hilo lililojaza umati wa jinsi na rika zote wakiwemo watoto lilijiri katikati ya wiki hii, maeneo ya Mji Mpya ndani ya chumba na kitanda cha wanandoa hao. 
Kikiwa kwenye mishe zake, kile kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers mkoani hapa kilipenyezewa kuwepo kwa ‘uovu’ huo ambapo hakikulaza damu.

ENEO LA TUKIO
OFM, ikiwa eneo la tukio ilijikusanyia madai mazito juu ya jamaa huyo kuwa amekuwa na kasumba ya kumhonga vyakula mke huyo wa mtu ambaye naye kwa kukosa uaminifu kwenye ndoa alijikuta akiingia mkenge hasa mumewe anapokuwa safarini kwa kuwa ni mtu wa kusafiri katika biashara zake binafsi.
Ilidaiwa kwamba, mwanamke huyo hutumia mwanya huo kumwingiza mchepuko wake huyo kwenye chumba na kitanda anacholala na mumewe kisha ‘kufanya yao’.

Baada ya kukolea huku mahaba niue yakitajwa na sauti ‘tamutamu’ zikisikika chumbani, majirani walikerwa na kitendo hicho cha jirani yao kudhulumiwa ‘mali’ zake ndipo wakaamua kumpa ‘ubuyu’ mume.
Ilisemekana kwamba, mume, akishirikiana na majirani aliowaomba ushirikiano, aliweka mtego ambapo alijifanya anasafiri kama kawaida.

Wananchi wakimshuhudia muuza genge huyo akihadhirika baada ya fumanizi.
Siku ya tukio, saa husika ilifika, kama kawaida jamaa alifika nyumbani kwa wanandoa hao kisha kuchoma chumbani kwa wanandoa tayari kwa kulicheza ‘segere’.
LAIVU NA SUTI YA KUZALIWA
Mwenye mke, akiwa chimbo alitonywa na majirani kuwa mambo ‘yamekwiva’ chumbani ndipo akawaibukia na kumkuta jamaa laivu akiwa mtupu. Haikujulikana kama ilikuwa ‘tayari au bado’.
Akiwa na hasira, mwenye mke alidaiwa kumshushia kipigo mgoni kilichomfanya kuloa damu chapachapa na baadaye kumtoa nje akiwa mtupu kisha kumtembeza mtaani kwenda nyumbani kwake huku ‘kadamnasi’ ikipiga kelele ‘watu weweee...”

Katika hali ya kushangaza, mwenye mke aliomba mkewe asipigwe picha akidai bado anampenda na hayuko tayari kumuacha. 
Kwa upande wake, jamaa huyo aliyedaiwa kufumaniwa alipohojiwa na OFM, aligoma kuzungumza na badala yake alificha uso kwa aibu.

KIKONGWE ALIYEKUTWA UCHI KWENYE NYUMBA YA MTU HUKO SHINYANGA AITAKA SERIKALI KUACHA KUKURUPUKA NA WAPIGA RAMLI.


SERIKALI imeshauriwa kutekeleza kwa uangalifu mkubwa adhima yake ya kupambana na waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli zinazodaiwa ni chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) kwa vile hatua hiyo inaweza kusababisha madhara makubwa kwa taifa.
 
Ushauri huo umetolewa na mmoja wa wazee maarufu mjini Shinyanga, Iddi Juma ambapo amesema serikali haipaswi kukurupuka katika kushughulikia suala la waganga wa jadi kwa vile baadhi yao wana umuhimu mkubwa kwa jamii na wamekuwepo nchini tangu enzi na enzi.
 
Juma alisema kuwadharau waganga wa jadi ni kutaka kusababisha matatizo yasiyo ya lazima yanayoweza kutokea nchini kwa vile wengi wao wana uwezo mkubwa wa kutibu baadhi ya magonjwa yaliyoshindikana kwa kutumia miti shamba na hata baadhi ya viongozi wakubwa serikalini na wanasiasa huwategemea waganga hao katika mambo yao mengi.
 
“Nimesikia serikali imetangaza hivi karibuni itaendesha kampeni ya kupambana na waganga wa jadi wanaopiga ramli chonganishi kwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, sipingani na kampeni hii, ombi langu kwa serikali iwe makini inapotekeleza kazi hii vinginevyo inaweza kutuletea madhara makubwa,”
 
“Waganga wa jadi ni watu muhimu katika jamii yetu, kuna magonjwa yanayoshindikana katika tiba za kitaalamu lakini wao wamekuwa wakiyatibu, magonjwa mengine bwana hayana tiba katika hospitali zetu, lakini ni rahisi mno kupata tiba yake kwa waganga wa jadi, kukurupuka na kuwakamata ni kujiletea matatizo,” 

"Hivi kweli kuna tiba yoyote ya majini au mapepo machafu katika hospitali zetu nchini? wanaopatwa na matatizo haya mara nyingi tunaona wanakimbizwa kwa waganga wa jadi, ndiyo wataalamu wa kuyatibu, na huko ni lazima mganga afanye mambo yake ili kubaini yametokea wapi, sasa tukiwakamata wenye matatizo haya watatibiwa wapi?" alihoji Juma.
 
Mzee huyo alisema yeye binafsi anao ushahidi baadhi ya viongozi wa kisiasa na wa kiserikali ambao wanategemea sana nguvu ya waganga wa jadi, na kwamba kutokana na hali hiyo ni wazi wale watakaokamatwa na kuchukuliwa hatua watakuwa ni wasiokuwa na mahusiano na viongozi wowote ndani ya serikali ama wanasiasa.
 
Alisema yapo mambo yanayoweza kufanywa na waganga hao kutokana na kutoridhishwa na hatua zitakazochukuliwa na serikali dhidi yao na hivyo kusababisha mtafaruku mkubwa nchini ambapo amesisitiza umuhimu wa kutumika kwa busara kubwa katika kuwabaini wanaojihusisha na upigaji ramli chonganishi badala ya kukurupuka kukamata ovyo.
 
“Hawa watu wasidharauliwe, maana wametajwa hata ndani ya vitabu vya mwenyezi mungu, kwa sisi waislamu ipo aya inayoelezea jinsi mambo ya kichawi yalivyofundishwa na malaika wawili, lakini mungu ametukataza kabisa binadamu tusijihusishe nayo kwani ni fitina juu yetu, hivyo ni muhimu tukawa makini katika kuwashughulikia,” alieleza Juma.

TAARIFA JUU MEYA MANISPAA MOROGORO NA WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI



Gari la Meya likiwa halitamaniki.
Wasamalia wakimuwahisha Hospital, Mmoja wa majeruhi mara baada ya kupata ajali eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe (wa kwanza kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro , Said Amanzi , wakipita eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.
Hili ndilo basi lililogongana na Gari ya Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo ,(45) akiwa amelazwa wodi namba tano ya daraja la kwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari yake SM 4151 ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam ,mbali na Meya huyo na watu wengine watatu ,Dereva Mwambala Ally (55), na waandishi wa habari , Anita Chali (30) pamoja na HUSSEIN Nuha (28) pia walijeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu. ( Picha na John Nditi).
Mwandishi wa habari,Anita Chali akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari waliyoipata,walipokuwa kwenye kazi na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akionesha eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kupimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.
 
Na John Nditi, Morogoro
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa Morogoro , Amir Nondo (45), dereva  na waandishi  wa habari wawili wamepata ajali   baada ya  gari walilokuwa wakisafiria kugongwa na basi la abiria lenye namba za usajili T 831 CEH, aina ya Scania mali ya kampuni ya Happy Africa na kujeruhiwa  sehemu mbalimbali za miili yao na kulazwa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
 
Tukio hilo lilitokea Januari 30, mwaka huu majira ya saa 9: 30 alasiri , eneo la Msamvu Mzambarauni darajani katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam, ambapo basi hilo lilikuwa likotokea mkoani Njombe.
 
Majina ya watu hao wengine waliojeruhiwa na kulaza katika wodi za daraja la kwanza katika hospitali ya rufaa ya mkoa , ni dereva wa gari la Meya, Mwambala Ally (55) , na waandishi wa habari ambao ni wapigapicha vituo vya televisheni , Anitha Chali (30) pamoja na Hussein Nuha (28).
 
Mstahiki meya huyo  aliyekuwa kwenye gari ya Halmashauri ya Manispaa hiyo  yenye namba za usajili SM 4151, ikiendeshwa na Mwambala  ambamo pia walikuwemo waandishi wa habari hayo na alikuwa katika msafara wa ziara ya kikazi ya mkuu wa mkoa huo,Dk Rajab Rutengwe.
 
Meya Nondo akizungumzia  ajali hiyo, akiwa wodini akipatiwa matibabu  ,sambamba na majeruhi wengine alisema baada ya kufika eneo la Mizambarauni, Darajani, lilichomoka pembeni basi la abiria ililokuwa likitokea Njombe kuelekea  Dar es  salaam, na kuligonga kwa mbele gari alilokuwemo.
 
Mashuhuda wa ajali hiyo  waliwaambia waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio,  kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni basi la abiria mali ya kampuni ya Happy Africa, kuingilia msafara huo wa mkuu wa mkoa uliokuwa ukielea mjini baada ya kukagua shughuli za ujenzi wa vyumba vya maabara na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Bigwa katika  Shule ya Sekondari Sumaye.
 
Mkuu wa mkoa kwa takribani wiki mbili amekuwa katika ziara katik halmashauri saba za mkoa huo kwa ajili ya kukagua shughuli za ujenzi na umaliziaji wa maabara tatu kwa kila shule ya skondari ya Kata na pia kutumia fursa hiyo kujitambulisha , kusikiliza kero na kuzipatia majawabu ya msingi.
 
Januari 29 na 30 mwaka huu ilikuwa ni zamu ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Shule ya sekondari Sumaye kilikuwa ni kituo chake cha mwisho katika ziara hiyo na baadaye kufanyika kwa majumuisho ya ziara hiyo Januari 31, mwaka huu mjini Morogoro.
 
Hata hivyo baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa ya mkoa , viongozi mbalimbali walifika kuwajulia hali  wakati wakiendelea kupatia matubabu na madaktari mbingwa wa hospitali hiyo, akiwemo Mganga mkuu wa mkoa , Godfrey Mtei.
 
Mstahiki Meya Nondo ameumia sehemu ya kichani na mkononi , wakati na mpiga picha Anita Chali, ameumia  kichwani, huku dereva pamoja na  Hussein wakiumia zaidi  kwenye paji la uso na kichwani huku Hussein akisaidiwa na mashine ya kupumulia (oxygen).
 
Kufuatia tukio hilo Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa mkoa imesema itatoa taarifa ya ajali hiyo  jumamosi ya  Januari  31, mwaka huu.

SOMA HAPA MAGAZETI YA LEO

.
.
Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC08838
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC08853
.
.

Ziko hapa kurasa za mwanzo na mwisho za Magazeti ya leo January 29, 2015

.
.
Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC08790
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC08804
.
.
.
.
DSC08807
.
.
.
DSC08811
.
.
.
.
.
DSC08810
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog