Home » »

ROSE MUHANDO JELA MIAKA SABA KWA TUHUMA ZA KUTOA MIMBA YA MIEZI SABA.


Rose Muhando.
KITENDO cha mwimbaji nyota wa muziki wa Injili, Rose Muhando (pichani) kudaiwa kutoa mimba ya miezi saba, endapo kitathibitishwa na mamlaka zinazohusika, kinaweza kusababisha kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 7 jela, Risasi Jumatano lina mkanda kamili.

Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili, Rose Muhando akiimba wakati akiwa mjamzito.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, ilidaiwa kuwa Rose, mwimbaji mwenye maskani yake mjini Dodoma, alikuwa ameitoa mimba aliyokuwa nayo, ambayo anadaiwa kupewa na mcheza shoo wake. Kama ingeenda salama na kujifungua, ingempatia mtoto wake wa nne.
Kufuatia madai hayo, gazeti hili lilifanya mawasiliano na wadau kadhaa, miongoni mwao wakiwa ni wanasheria, wanamuziki wenzake na viongozi juu ya ishu hiyo iliyoushtua ulimwengu wa Injili.
Mwanasheria mmoja maarufu nchini, ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa sababu alizodai ni za kimaslahi, alisema kutoa mimba ni kosa kisheria na wahusika, akiwemo mama na daktari aliyeshiriki kukamilisha tukio hilo, wanapaswa kushtakiwa na kuhukumiwa.

“Inategemea, kama alitoa mimba kwa sababu za kimatibabu, yaani ili afya yake iwe sawa ni lazima atoe ujauzito alionao, hilo siyo kosa, lakini kama alitoa kwa sababu nyinginezo nje ya hapo, ni kosa la jinai linalostahili adhabu.
“Kwa mujibu wa Sheria za Kanuni ya Adhabu sura ya 16, kifungu cha 150, daktari anayehusika na kosa hilo adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela na mama aliyetolewa ujauzito huo, kwa mujibu wa kifungu cha 151, anastahili kifungo cha miaka saba jela,” alisema mwanasheria huyo.
Kuhusu sababu za kumfunga kwa miaka mingi daktari badala ya mama aliyetaka kutolewa, ‘lawyer’ huyo alisema hii inatokana na kiapo ambacho madaktari huapa ambacho kinawataka kulinda uhai wa mtu na pia ni kukiuka maadili ya kazi yao.
“Mahakama itakuwa kali zaidi kwa madaktari kwa sababu ya dhamana ya kiapo chao. Huu unakuwa ni mfano kwa madaktari wengine ili wasimamie maadili na viapo vyao,” alisema mwanasheria huyo.
Katibu wa Chama Cha waimba Injili, Stella Joel, alipoulizwa kuhusu maoni yake juu ya kadhia hiyo, alisema chama chao hakina taarifa za tukio hilo, lakini wanaweza kuchukua hatua kama Polisi watalifanyia kazi jambo hilo kwa vile ni kosa la kijinai.

“Kutoa mimba ni kosa la Jinai, kwa hiyo kama Polisi watalifanyia kazi, sisi tutatoa tamko na kuchukua hatua, kwa sasa hatuna la kufanya, tunasikia katika vyombo vya habari na mitandao, tukimuuliza anakataa,” alisema.
Waimbaji wenzake, Bahati Bukuku na Christina Shusho walionyesha kushangazwa na tukio hilo, wakidai limewashtua na halikutarajiwa.
“Rose ni mtu mzima, kama kweli tukio hili lipo, basi huo ni uamuzi wake na Mungu wake, inategemea na mapatano yao, kila mtu ana maamuzi yake ila nimeshtushwa sana,” alisema Bahati Bukuku.
Shusho alisema jambo hilo ni baya na kosa kisheria, lakini hata hivyo ni suala binafsi linalomhusu mhusika. 
Rose Mhando mwenyewe alitafutwa katika simu yake ya mkononi ili kusikia kauli yake juu ya suala hilo, lakini zaidi ya mara nne, simu yake iliita hadi kukatika pasipo kupokelewa.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog