Home » » YAYA TOURE HUYOOOO INTER MILAN(PICHA)

YAYA TOURE HUYOOOO INTER MILAN(PICHA)


Boss wa Inter Milan Roberto Mancini ametangaza nia ya kumtaka kiungo wa  Manchester City Yaya Toure huku akikanusha juu ya uvumi wa nia yake ya kutaka kumsajili Lucas Leiva wa Liverpool.
Mancini anapata kiburi cha uhakika wa kumsajili Yaya Toure ambaye ana umri wa miaka 31, kwa sababu yeye ndiye aliye mleta Mana City akitokea Barcelona Mwaka 2010, na yeye ndiye aliye mtengeneza mpaka sasa ni mchezaji anayeng'aa katika ligi kuu Uingereza.
Aidha nyota huyo wa Ivory Coast hivi karibuni alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema kuwa maisha yake ya soka kwa miaka inayokuja hayaeleweki kwamba atakuwa klabu gani.
Hata hivyo gharama la dili hilo itakuwa kubwa kiasi kwamba itawawia vigumu Inter Milan kuipata saini ya mwanandinga huyo.
Lakini kuhusiana na gharama Mancini amenukuliwa akisema kuwa Toure atafurahia maisha ya San Siro "Nilimleta mimi Man City hivyo namfahamu na yeye ananifahamu vilivyo", "Nimchezaji mzuri katika wanasoka duniani lakini yupo Man City kwa muda".

Yaya Toure is not planning to end his two-year association with Manchester City Roberto Mancini akitembea na Yaya Toure wakati alipokuwa Manchester City.
Na Caunter Mgaya
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog