Home » » Kigogo wa BoT apandishwa kizimbani kwa jaribio kuua polisi

Kigogo wa BoT apandishwa kizimbani kwa jaribio kuua polisi

MSHAURI wa masuala ya ulinzi katika Benki Kuu (BoT), Shaban Ndosi (39) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kujaribu kumuua ofisa wa Polisi.

Ndosi alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema.

Wakili wa Serikali, Janeth Kitali alidai kuwa Oktoba 21, 2014 katika eneo daraja la Selander karibu na taa za kuongoza magari, alijaribu kumuua askari Polisi, Koplo Salehe.

Hakimu Lema alisema mshitakiwa hakutakiwa kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na upelelezi umeshakamilika hivyo kesi itahamishiwa Mahakam Kuu.

Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika waliosaini hati ya dhamana ya Sh milioni mbili, pia alitakiwa kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria.

Kesi hiyo itatajwa tena Februari 23 mwaka huu
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog