Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Hellen
Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa kuhusu
changamoto za utekelezaji wa sheria ya kura ya maoni ya Katiba. Kulia ni
Mratibu wa Katiba wa LHRC, Anna Henga na Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala, Ezekiel Massanja.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo
Wapiga picha na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
KITUO
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kina wasiwasi na
mchakato wa kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika kwa sabau ya muda
mdogo ulibaki ikizingatiwa daftari la wapigakura halijafanyiwa
marekebisho pia watanzania wengi hawana uelewa na katiba
iliyopendekezwa.
Kituo
kimetoa mapendokezo kwa Serikali kuahirisha tarehe ya kupiga kura ya
maoni kwa kile kilichodaiwa katiba inayopendekezwa inamapungufu na
yasiporekebishwa muda huu yanaweza kuathiri kura ya maoni na kuwakosesha
watanzania wengi kushiriki haki yao kikatiba.
Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, DK.
Hellen Kijo- Bisimba alisema kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa
kufuatilia mchakato wa katiba, kubaini mapugufu mengi likiwemo la muda
mdogo na wananchi wengi kutoelewa vizuri katiba inayopendekezwa.
"Mchakato wa kura ya maoni unaenda kukamilika Februari 28 kwa mjibu wa
sheria ya kura hiyo.Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapaswa kuboresha daftari
la wapiga kura ndipo kura ipigwe, ukizingatia zimebaki siku takribani
25 kufikiaki hitimisho,sisi tunaona kuna changamoto ya muda na ni vyema
zoezi hilo lisongezwe mbele,"alisema.
Aliongeza kuwa vifaa vya BRV vinavyotarajiwa kutumika kwa mara ya
kwanza na tume ya uchaguzi vimeonesha changamoto katika uchaguzi wa
Serikali za mitaa na hivyo kituo hicho kinawasiwasi na mchakato mzima wa
upatikaji wa katiba iliyo bora.
"Kifungu cha 10 katika katiba inayopendekezwa kimezungumzia vituo vya
kupigia kura, kwamba vitapangwa kulingana na maeneo yaliyo na watu wengi
katika maeneo husika wasiwasi wangu hapa tume inaweza kutotumia majimbo
ya zamani na kutengeza majimbo mpya,"alisema.
Bisimba alisema changamoto nyingine katika mchakatio huo ni Usajili wa
kamati za kura ya maoni katika kuikubali au kuikataa kura hiyo katiba
inaelekeza kamati ni lazima ipeleke maombi kabla ya siku 21 kupigwa kwa
kura ya maoni.
"Utaratibu ambao sisi kulingana na uzoefu wetu wa kufanya kazi tunaona
haya ni masharti magumu yanayoekekezwa kwenye kamati za kura, kwani
inawataka pia kueleza vyanzo vya mapato yao kitu ambacho kinaweza
kusababisha kamati zingine kutopata usajili,"alisema.
Dk.Bisimba aliongeza kuwa changamoto ambayo kituo kinaona kuwa ni kiini
macho ni pale inapoelezwa kwamba wanzazibar waishio Tanzania bara
wakipiga kura kura zao zitahesambiwa upande wa zanzibar.
0 comments:
Post a Comment