Home » »

MAJANGA..!! JAMAA ALIYEIBA RADIO CALL YA POLISI, AJINYONGA AKIWA KITUO CHA POLISI



Mtuhumiwa mmoja aliyejulikana kwa jina la Bosco Ndunguru(40) aliyekuwa akishikiliwa katika kituo kikuu cha polisi wilayani Mbinga mkoani Ruvuma amekutwa akiwa amejinyonga kituoni hapo kwa kutumia shati alilokuwa amaelivaa wakati akiwa mahabusu.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema mtuhumiwa huyo alikuwa anashikiliwa kituoni hapo kwa tuhuma za kuvunja jingo la polisi na kuiba radio call ya kituo hicho mwaka jana na kisha kutoroka na jeshi lilimsaka na kufanikiwa kumkamata na kumweka mahabusu ili kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Amesema chanzo cha awali kuhusu tukio hilo lililotokea Januari 23 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi mtuhumiwa huyo alisikika akilalamika sana huku akilia na kudai kuwa ndugu zake hawampendi wakati akiongea na wenzake mahabusu walimokuwa wamewekwa.

Kamanda Msikhela amesema mara baada ya askari waliokuwa zamu kumaliza muda wao waliingia wengine na kabla ya kutoka kazini askari hao walikabidhiana kituo pamoja na mali zilizopo kituoni hapo mtuhumiwa huyo pamoja na watuhumiwa wengine watatu wenye makosa tofauti wakiwa mahabusu na ndipo mtuhumiwa Bosco Ndunguru alitumia muda huo kutoka na kujifanya akielekea chooni na kuingia chumba cha jirani na mahabusu ambacho kilikuwa hakina mtu na kujitundika kwa kutumia shati.

Amesema aliweza kufanikisha kitendo hicho kwa kujitundika kwa kutumia shati na kwa kujitundika kwenye nondo ya mlango wa chumba hicho mpaka alipogunduliwa na mmoja kati ya watuhumiwa waliokuwepo ndani na kutoa taarifa kwa askari waliokuwa zamu ilipofika saa moja asubhi Januari 24 mwaka huu.

Amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na mganga kutoka hospitali ya wilaya ya Mbinga waliufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na kukabid
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog