SAKATA LA ESROW KUENDELEA TENA LEO

MBUNGE wa Mwibara (CCM), Alphaxard Kangi Lugola wakati akichangia katika Ripoti ya PAC kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow bungeni leo, ameomba kuchangia  akiwa amevaa 'Kininja' ili kutowaangalia usoni wahusika wa sakata hilo. 

Mbali na kuvaa hivyo, Lugola pia aliomba kama kanuni zinaruhusu achangie tena akiwa amevaa nguo za chama chake cha CCM ili kuonyesha kuwa CCM haiungi mkono vitendo viovu japo alikataliwa na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Zungu.


BON MWAITEGE AJA NA KITU KIPYA CHA DAKIKA 45 SOMA MWANANGU AKISHIRIKIANA NA BAHATI BUKUKU


Mwanzoni mwa wiki hili mwanamziki wa nyimbo za injili bon mwaitege amesikika redioni kuwa anatarajia kuja na ujio mpya baada ya kutamba na albamu ya mama ni mama sasa amekuja na wimbo ambao unajulikana kama {soma mwanangu} akiwa ameshirikiana na bahati bukuku,
akizungumza na gospel za iringa na habari bon amesema kuwa wimbo huo ambao umelenga zaidi kwa upande wa elimu ameuandaa ili watanzania hususa wanafunzi watambue umhimu wa elimu katika nyakati za sasa,
aidha bon amesema kuwa video ya wimbo huo inatarajia kukamilika ndani ya wiki mbili zijazo ikiwa na dk 45 hivyo wanainchi wajiandae kuipokea.

HATIMAYE MWIMBAJI NA MWALIMU WA KWAYA YA LULU GEOGY NJABILI AZIKWA LEO JIJINI MBEYA

Marehemu George 'Bonge' Njabili
Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Bima karibu na Shule ya St Mary's ambapo watu mbali mbali wanaweza kufika kutoa pole kwa familia ya Marehemu.

Ratiba ya kuuaga mwili itaanza kesho saa 4 kamili aubuhi nyumbani kwa marehemu hadi hapo itakapo ishia kisha msafara utaanza kuondoka kuelekea katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mtoni ambapo watu watapata nafasi ya kuaga tena kabla ya safari ya kuupeleka mwili Tukuyu, mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa mtoa ratiba, Benjamin Kihogo ambaye pia ni mwalimu wa kwaya ya Mtoni, ameeleza kwamba pia watu wanaweza kuchangia kwa kupitia namba ya kaka wa marehemu Tigopesa 0654 02 14 23 Mpesa 0754 46 41 02.
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/11/ratiba-ya-maazishi-ya-marehemu-george.html#sthash.HmUSumMi.dpuf
Na Joseph Msami,
GK Author.
Marehemu George bonge, Joseph Msami na Ritha Chuwalo.
Nimesikitishwa sana na msiba wa huyu mutumishi na rafiki yangu! Nilipomwona zaidi ya miaka kumi iliyopita nilimpenda na kumwomba awe rafiki yangu. Wakati huo hata simu za mikononi zilikuwa siyo nyingi akanipa no ya mezani ofisini kwake.
Niliwasiliana naye sana na hata mara nyingine nahisi nilikuwa namsumbua. Lakini nimejifunza sana unyenyekevu wake mkuu ambao siwezi kuusahau na namna alivyokuwa akimpokea mtu yeyote utadhani wanafahamiana naye kwa muda mrefu!

Imeniuma sana kumpoteza mtu huyu muhimu. Pia nimetiwa changamoto ya kujiandaa muda wowote (Zaburi119:1-5) ili andiko likitimia niwe tayari.

Natamani ningekuwa Dar nishuhudie safari ya mwisho ya rafiki yangu. Nawaombea sana hususani shemeji (mke wa George). Mungu hatawapungukia.
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/11/kwaheri-rafiki-george-nasi-tunafuatia.html#sthash.Ner8dmWg.dpuf

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Search This Blog