AIBU KUBWA! MUUZA GENGE ACHEZEA KICHAPO KWA KUNASWA NA MKE WA MTU
Aibu kubwa! Muuza
genge mmoja kwenye Soko la Mji Mpya mjini hapa ambaye jina
halikupatikana mara moja, amejikuta akichezea kichapo kwa madai ya
kunaswa na mke wa mtu kisha kutembezwa mtupu mtaani.
Muuza genge aliyechezea kichapo baada ya kunaswa na mke wa mtu na kutembezwa mtupu mtaani.
Fumanizi
hilo lililojaza umati wa jinsi na rika zote wakiwemo watoto lilijiri
katikati ya wiki hii, maeneo ya Mji Mpya ndani ya chumba na kitanda cha
wanandoa hao.
Kikiwa
kwenye mishe zake, kile kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM)
cha Global Publishers mkoani hapa kilipenyezewa kuwepo kwa ‘uovu’ huo
ambapo hakikulaza damu.
ENEO LA TUKIO
OFM,
ikiwa eneo la tukio ilijikusanyia madai mazito juu ya jamaa huyo kuwa
amekuwa na kasumba ya kumhonga vyakula mke huyo wa mtu ambaye naye kwa
kukosa uaminifu kwenye ndoa alijikuta akiingia mkenge hasa mumewe
anapokuwa safarini kwa kuwa ni mtu wa kusafiri katika biashara zake
binafsi.
Ilidaiwa
kwamba, mwanamke huyo hutumia mwanya huo kumwingiza mchepuko wake huyo
kwenye chumba na kitanda anacholala na mumewe kisha ‘kufanya yao’.
Baada
ya kukolea huku mahaba niue yakitajwa na sauti ‘tamutamu’ zikisikika
chumbani, majirani walikerwa na kitendo hicho cha jirani yao kudhulumiwa
‘mali’ zake ndipo wakaamua kumpa ‘ubuyu’ mume.
Ilisemekana
kwamba, mume, akishirikiana na majirani aliowaomba ushirikiano, aliweka
mtego ambapo alijifanya anasafiri kama kawaida.
Siku ya tukio, saa husika ilifika, kama kawaida jamaa alifika nyumbani
kwa wanandoa hao kisha kuchoma chumbani kwa wanandoa tayari kwa
kulicheza ‘segere’.
LAIVU NA SUTI YA KUZALIWA
Mwenye
mke, akiwa chimbo alitonywa na majirani kuwa mambo ‘yamekwiva’ chumbani
ndipo akawaibukia na kumkuta jamaa laivu akiwa mtupu. Haikujulikana
kama ilikuwa ‘tayari au bado’.
Akiwa
na hasira, mwenye mke alidaiwa kumshushia kipigo mgoni kilichomfanya
kuloa damu chapachapa na baadaye kumtoa nje akiwa mtupu kisha kumtembeza
mtaani kwenda nyumbani kwake huku ‘kadamnasi’ ikipiga kelele ‘watu
weweee...”
Katika hali ya kushangaza, mwenye mke aliomba mkewe asipigwe picha akidai bado anampenda na hayuko tayari kumuacha.
Kwa upande wake, jamaa huyo aliyedaiwa kufumaniwa alipohojiwa na OFM, aligoma kuzungumza na badala yake alificha uso kwa aibu.
0 comments:
Post a Comment