Home » » STENDI YA IPOGOLO IRINGA YAFUNGWA BAADA YA MTOTO KUGONGWA NA KUFARIKI, MOTO WACHOMWA BARABARANI

STENDI YA IPOGOLO IRINGA YAFUNGWA BAADA YA MTOTO KUGONGWA NA KUFARIKI, MOTO WACHOMWA BARABARANI


 
UTAMADUNI wa wananchi kujichukulia sheria mkononi unazidi kushabikiwa na kuchochea ghasia kila mahali nchini hali inayoweza kusababisha madhara makubwa pamoja na uvunjifu wa amani.

Siku moja baada ya madereva kugoma na kusababisha hadha kubwa kwa abiria na watumiaji wa vyombo vya usafiri katika maeneo mbalimbali nchini na hasa hasa jijini Dar es Salaam kulikoshuhudiwa jeshi la Polisi likilazimika kutumia mabomu ya machovu kuwatawanya waliokuwa wanafanya fujo, kuchoma matairi barabarani na hata kuiba mali na kuharibu magari ya watu wengine wakati mgomo huo ukiendelea:

Leo hii katika eneo la stendi ya Ipogolo, vijana wenye hasira kali wamechoma  matairi chakavu barabarani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara iendayo katika stendi hiyo, baada ya dereva na gari ambalo hata hivyo halikujulikana mara moja kumgonga mtoto aliyekuwa akivuka barabara hiyo na kufariki papo hapo.

Stendi ya mabasi Ipogolo imefungwa na hadi tunakwenda mitamboni hakuna gari lililokuwa linaingia au kutoka.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog