IDADI KAMILI YA WALIOKUFA KWA AJALI ZOTE ZILIZOTOKEA HIVI KARIBUNI HII HAPA.
Jumla
ya watu 103 wamepoteza maisha katika matukio makubwa ya ajali
yaliyotokea kwa kipindi cha mwezi mmoja katika maeneo mbalimbali hapa
nchini huku idadi ya majeruhi katika ajali hizo ikifikia watu 138 na
baadhi ya majeruhi wakibaki na ulemavu wa kudumu.
Watu
103 kupoteza maisha na watu 138 kujeruhiwa ikiwemo wengine kupata
ulemavu wa kudumu imetokea kwa kipindi cha mwezi mmoja tu katika maeneo
mbalimbali hapa nchini,huku chanzo kikubwa cha ajali hizi zilizopoteza
maisha ya watanzania imedaiwa kusababishwa na uzembe wa baadhi ya
madereva.
Jeshi
la polisi kikosi cha usalama barabarani mbali na kubaini vyanzo vya
ajali hizo zilizotokea katika maeneo mbalimbali nchini kwa kutaja kuwa
ni uzembe wa baadhi ya madereva,tatizo la mwendo kasi,ubabe wa baadhi ya
madereva kwa magari madogo,mkuu wa kikosi cha usalama barabarani
Mohamed Mpinga,amelazimika kuweka wazi idadi ya vifo vilivyotokea katika
ajali mbalimbali kuanzia mwezi january mwaka huu,ambapo watu wengi
wamepoteza maisha.
Baadhi
ya wanasheria wamesema kuna udhaifu mkubwa katika sheria
inayotumika,kwani licha ya madereva na wamiliki wa mabasi na magari
binafsi wakugundulika kusababisha watu kupoteza maisha kutokana na
uzembe wao,hakuna sheria kali inayotumika kuwabana mbali na kutozwa
faini ndogondogo huku ndugu wa marehemu waliopoteza maisha katika ajali
hizo pamoja na majeruhi hasa wale waliachwa na ulemavu wa kudumu
wakibaki njia panda bila kupewa fidia yeyote na wamiliki wa vyombo
hivyo.