Home » »

BODABODA AFA KWA KUCHINJWA, NDUGU WAZIKA MGOMBA, UTATA WATAWALA

TUKIO la aina yake! Dereva wa bodaboda aliyejulikana kwa jina la Alex Wilson amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa na kuporwa pikipiki lakini cha ajabu, siku ya mazishi yake kaburini kukazikwa mgomba baada ya mwili kuzuiwa usizikwe, Uwazi limechimba kisa kamili.

Marehemu Alex Wilson enzi za uhai wake.

Ilikuwa Aprili 8, mwaka huu katika maeneo ya Mbezi Beach karibu na Kiwanda cha Rafia, Alex ambaye ni mwenyeji wa Sumbawanga mkoani Rukwa, aliuawa kwa kuchinjwa mfano wa kuku.Baada ya kifo hicho, madereva bodaboda wenzake waliungana na kutafuta ndugu wa karibu ili kuwajulisha kilichomkuta Alex.

Inadaiwa kuwa, katika kutafuta alikokuwa akiishi marehemu huyo, wenzake walifanikiwa kupapata na kumkuta mtoto wa mama mwenye nyumba ambapo walimuonesha picha za enzi za uhai wa Alex naye ndugu huyo alikiri kwa kusema ni kaka yake.

Walimuuliza mtoto huyo aliko mama yake akasema yuko safarini Sumbawanga kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka.
“Tulimwomba namba ya simu ya mama yake, akatupa. Tulipompigia alisema kweli anamtambua marehemu lakini yeye yuko Sumbawanga,” alisema mmoja wa madereva bodaboda hao.

Wananchi wakipeleka mgomba makaburini.

Inadaiwa kuwa, bodaboda hao walimtaka mama huyo kutoa tamko juu ya kuusafirisha mwili wa Alex kwenda Sumbawanga au kuuzika jijini Dar ambapo alisema waende serikali ya mtaa kwa ajili ya kupata utaratibu kisha wamzike.

“Siku iliyofuata, yaani Aprili 9, mwaka huu, tukiwa na baadhi ya ndugu wa mbali wa Alex tulikwenda Kituo cha Polisi Afrikana (Dar) kuomba kibali cha mazishi, lakini ikabidi polisi wafanye mawasiliano na yule mama aliye Sumbawanga.

“Polisi walimpigia simu na kuweka loud speaker (spika kwa sauti ya nje) wakimtaka mama huyo afike Dar haraka kwa mazishi ya mtoto wake au waruhusu mtoto wake azikwe.“Lakini yule mama alijibu kuwa, wasijaribu kufanya kitendo chochote cha mazishi kwa vile anajua kuwa mwanae huyo hajafa na anajua alipo.

Kaburi likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.

“Mama alisema watu wakifanya lolote watakiona maana yeye anatoka Sumbawanga, hivyo zoezi la kuendelea na taratibu za maziko zikakwamia hapo,” alisema bodaboda mmoja.Aliendelea kusema kuwa, wakati wanafanya utaratibu wa kupata kibali tayari walishachimba kaburi kwa ajili ya kumhifadhi marehemu. “Lakini baada ya mama kujibu vile, polisi walifanya mawasiliano na viongozi wa juu na kuzuia maziko hadi ndugu sahihi wapatikane na hivyo mwili wa maremu upo Hospitali ya Mwananyamala (Dar) ukisubiri.”

Baada ya hapo bodaboda hao kwa kushirikiana na ndugu wa mbali, walilazimika kukata mgomba na kuuzika kaburini badala ya mwili wa marehemu.Mgomba huo ulizikwa katika Makaburi ya Kinzidi, Aprili 9, mwaka huu kwa kile kilichodaiwa kuwa, kuacha kaburi wazi wakati lilishachimbwa kwa ajili ya maziko ni uchuro kwa wengine walio hai.

Mgomba ukiwa kwenye kaburi.

Jumamosi iliyopita, Uwazi lilifanya jitihada na kumpata mama huyo kwa njia ya simu ambapo alijitambulisha kwa jina la mama Dickson na kusema yupo Mtaa wa Majengo wilayani Sumbawanga, Rukwa.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na marehemu Alex, mwanamke huyo alisema:

“Ni kweli Alex namfahamu na tulifahamiana Dar es Salaam na hii ni kutokana na kunifahamu mimi ni mtu wa Sumbawanga hivyo siku za nyuma alikuja nyumbani kwangu na kujitambulisha, mimi nilimchukulia kama mwanangu.

Mgomba ukifukiwa.

“Ilifika mahali akawa ananiita shangazi, mahusiano yalikuwa ni makubwa kutokana na kutoka sehemu mmoja yeye alinichukulia kama ndugu yake wa karibu.“Mbali na kutoka sehemu mmoja sina undugu na Alex.”
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog