Home » »

Vyama Vingi vya Siasa Vinatamaa ya Madaraka na Vyeo - Zitto Kabwe


Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparency ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kuwa vyama vingi vya siasa nchini,vinasumbuliwa na uroho wa madaraka pamoja na vyeo.

Aliongeza kuwa vyama hivyo katika mikutano yake vimekuwa vikiacha kueleza matatizo yanayowakabiliwananchi badala yake ni kutukana mwanzo mwisho.

Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wakazi wa Mji wa Maswa mkoani Simiyu, katika uwanja wa Madeco, wakati wakihitimisha ziara yakukitambulisha chama katika mikoa 12 nchini.

Alisema uroho wa kutaka madaraka na vyeo kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa vyama hivyo, limekuwa tatizo kubwa na kuvifanya kushindwa kupambana kutetea hali za Watanzania ambao niwengi wao ni maskini wa kupindukia.

“Baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini kazi yao ni matusi tu katika mikutano yao pamoja na kutambiana, vinashindwa kuwaeleza wananchi wanavyonyonywa na rasilimali zao zinavyonufaisha wachache, lakini pia tamaa ya madaraka pamoja vyeo katika vyama hivyo ni tatizo,” alisemaZitto.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog