Home » »

POLISI, MAJAMBAZI WARUSHIANA RISASI, WAWILI WAUAWA


WATU wawili akiwemo jambazi mmoja wamefariki dunia na wengine kunisurika kuuawa katika tukio la lililotokea juzi, mjini Mafinga mkoani Iringa wakati majambazi yakirushiana risasi na askari wa jeshi la Polisi.

Risasi hizo zilipigwa wakati Polisi hao wakijaribu kuokoa fedha za mfanyabiashara Salama Semwaiko zilizoporwa na majambazi wawili waliotumia pikipiki wakati wakifanya uporaji huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema mfanyabiashara huyo aliporwa fedha hizo juzi majira ya saa 2.45 asubuhi alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda kwenye biashara zake.

Tukio hilo la kusikitisha lilovuta hisia za watu wengi na kufanya baadhi kuzimia wengine  kukimbia hovyo na  kujifungia ndani kwa ajili ya kuokoa maisha yao  lilitokea katika eneo la Kinyanambo B, nje kidogo ya mji wa mafinga. 

Kamanda Mungi alisema “akiwa katika gari yake akielekea kwenye biashara zake mjini mafinga,  mfanyabiashara huyo alisimamishwa na mtu mmoja aliyekuwa amevaa koti jeusi na baada ya kusimama alimtolea silaha na kumtaka atoe fedha na vitu vyote vya thamani alivyoko navyo .”

“Baada ya kuona hana msaada mfanyabiashara huyo alijikuta akilazimika kutoa Sh 700,000 alizokuwa nazo, simu ya mkononi na baadaye ilitokea pikipiki ambayo haikufahamika namba za usajili na kumpakia mtu huyo na kuanza kukimbilia eneo la kinyanambo,” alisema. 

Alisema mara baada ya majambazi hao kutoweka jeshi la polisi lilipewa taarifa na kuwahi eneo la tukio na kwa kushirikiana na wanachi walianza kuwakimbiza majambazi hao na ndipo majibizano ya risasi yalipoanza.

Katika hekaheka hiyo, Kamanda Mungi alisema Said Ngudi (25) ambaye ni mwanajeshi wa JKT Makutopola aliuawa kwa bahati mbaya wakati akisaidia kupambana na majambazi hao.

“Kijana huyo alipigwa risasi ya kifuani upande wa kushoto na kufariki dunia papohapo  lakini wanachi  wananchi na askari hawakurudi nyuma kwani waliendelea kupambana na majambazi  hao,” alisema.

Kamanda  Mungi alisema katika majibishano hayo hatimaye polisi walifanikiwa kumpiga risasi ya kwenye paji la kushoto jambazi aliyempora mfanyabiashara huyo na hatimaye wanachi walimvania na kumpiga kwa mawe kabla hajaokolewa na kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.

Katika tukio hilo ambalo jambazi mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki alitokomea kusikojulikana,  jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata bunduki moja aina ya SMG na kuwashukuru wanachi kwa ushirikiano wao katika ulinzi shirikishi.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog