Home » »

  Vurugu Zaibuka Bungeni.......Wapinzani Wamtuhumu Spika Kuilinda Serikali, Bunge Laahirishwa hadi Mchana. Video Ya Tukio Hilo Iko Hapa.


Kikao cha  Bunge kimevunjika muda mfupi uliopita baada ya kutokea vurugu za maneno kufuatia wapinzani kutaka Waziri Mkuu atoe taarifa juu ya mwenendo wa kura ya maoni ya katiba mpya april 30,2015.

Kutokana na vurugu hizo za dakika kama 10 hivi Spika Anna Makinda amesitisha gafla shughuli za bunge hadi mchana.

Hali likuwa hivi:

Mnyika: Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima.

Mpaka sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili ni la dharura na lilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie.Tunaomba majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano.

Spika Makinda: Hoja hii inafanana na ile ya kwanza(  Hoja  ya  mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo ambaye  alipendekeza kura ya maoni ya katiba  inayopendekezwa isogezwe mbele  na  badala  yake  kuwe  na  katiba  ya  mpito  kuelekea  uchaguzi  mkuu)

Baada  ya  kauli  hiyo, Mnyika  na  wabunge  wa  upinzani  walianza  kupiga  kelele  bungeni  wakidai  kuonewa  huku  wakimtuhumu  Spika  makinda  kuibeba  serikali.

Hata hivyo, Spika  hakuonesha  kutishwa  na  kelele  hizo  na  badala  yake  alimtaka  katibu  wa  Bunge  atoe  mwongozo  wa  kile  kinachofuata.

Katibu  alisimama  na  kuanza  kusoma  miswada  ya  habari ambapo  wapinzani  nao  walisimama  na  kuzidisha  kelele  huku  wakisema: "Tunataka majibu..Tunataka majibu. Tumechoka kuburuzwa..Makinda kwanini unailinda Serikali.??!!!

Hali  hiyo  ikamlazima  Spika  Makinda  Kuliahirisha  Bunge  hadi  mchana.

Tazama  Video  hapo  chini.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog