Home » »

MAKUMI ELFU WAJITOKEZA KUIOMBEA SYRIA AMANI

Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye maombi ya kufunga ya masaa manne kwa ajili ya taifa la Syria. ©AP
Makumi elfu ya watu walijitokeza siku ya Jumamosi katika kuitikia wito wa Papa Francis, ili kuombea amani taifa la Syria, ambalo limekuwA katika vita ya wenyewe kwa wenyewe, ambapo na kwa sasa Marekani wanataka kushambulia taifa hilo kutokana na kusadikika kutumia silaha za sumu huko Damascus mnamo Agosti 21.

Papa Francis alitumia wasaha huo kuomba kimya kimya, ambapo wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro walibeba bendera za Syria pamoja na vipeperushi vilivyosomeka, "Achaneni na Syria", mengine yakisomeka, "Msiishambulie Syria".

Maombi haya yaliyotangazwa na Papa tarehe mosi Septemba, yaliitikiwa na maaskofu maeneo mbalimbali kuanzia Italy, Cuba, na sehemu nyinginezo, ambapo pia huko Damascus, mufti mkuu alimshukuru Papa kwa jitihada zake na kuwaalika waislamu kufunga na kuomba kwa pamoja na wenzao walioko Roma.
Papa Francis akiendelea kusali kwenye mfungo huo wa wa kuiombea Syria. ©AP
"Wahindu, Wabuddha, na hata wasio na dini wote walijitokeza kufunga kwa ajili ya suala hilo. haya ni mafanikio makubwa sana". Anasema mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Anata.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog