Home » »


 Habari kutoka mkoani Ruvuma zinasema kuwa wanafunzi 16 wa shule ya sekondari ya Misheni ya  Kigonsela wilaya ya Mbinga wanadaiwa kupoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa vibaya katika gari linalomilikiwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo.


Ajali hiyo imetokea jana katika eneo la kijiji cha Kigonsela kata ya Kigonsela  baada ya gari dogo aina  ya Landrover 110
lenye milango mitano kushindwa kupanda mlima na kupinduka kwenye korongo kisha kuwaka moto.

Wanafunzi hao walikuwa wanatoka kwenye shamba la shule kurudi shule,walifuatwa na mkuu wa shule hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Ngaiwona Nkondola aliyeongea na kamanda wa polisi mkoani humo,huenda ajali hiyo imetokana na kuzidiwa kwani ndani ya gari hilo kulikuwa na wanafunzi 16 ambao wote wameteketea kwa moto pamoja na mwalimu wao huku juu ya gari (keria) wakiwa wamekaa wanafunzi zaidi ya 20 ambao wamejeruhiwa vibaya.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog