..!! MELI YAZAMA IKIWA NA WATU ZAIDI YA 450, CHANZO CHATAJWA KUWA NI UPEPO MKALI NA MVUA KUBWA

Meli ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imezama baada ya kukumbwa na upepo mkali katika Mto Yangtze kusini mwaChina.
Kwa mujibu wa shirika la
habari la serikali Xinhua watu wanane wameokolewa mpaka sasa na kazi
inaendelea ya kuwaokoa abiria wengine.
Waziri Mkuu Li Keqiang anaelekea katika eneo la tukio.
Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mashariki mwa mji wa Nanjing kwenda Chongqing kusini magharibi ilipozama.
Meli hiyo,
Dongfangzhixing - au Nyota ya Mashariki - ilikuwa imewabeba abiria wa
Kichina 405, wafanyakazi watano wa shirika la usafiri na wafanyakazi 47
wa meli hiyo.
Nahodha na mhandisi
mkuu, ambao ni miongoni mwa waliokolewa wamekaririwa wakisema kuwa meli
ilikumbwa na kimbunga na kuzama haraka.
Kazi ya uokoaji imekwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa. Meli hiyo ilizama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.
Kwa mujibu wa shirika la
utangazaji la serikali ya China, meli hiyo inamilikiwa na Shirika la
Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha shughuli za utalii katika
maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.
Waliokuwa katika meli
hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa
katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya Shanghai.
Habari zinasema meli hiyo imepinduka.
Watu ishirini na wawili
waliufa katika mto huo mwezi Januari, wakati boti iliyokuwa katika
majaribio kuzama karibu na Zhangjiagang, katika jimbo la Jiangsu.
0 comments:
Post a Comment