Home » »

Alipandikizwa uso wa marehemu baada ya kupata ajali mbaya…

dada
Ajali nyingi duniani zimekua zikisababisha vifo vya watu wengi huku zikiacha wengine wakiwa na ulemavu wa maisha ambao huwasababishia kupoteza mwelekeo wa maisha yao na kukata tamaa kabisa.
Pamoja na wengi kubaki na ulemavu, lakini pia madaktari wamekuwa kijitahidi kadri wawezavyo kuwarudisha watu hao katika hali zao lakini moja ya tukio la kushangaza ni la kijana Richard Norris ambaye alipata ajali mbaya na kumpelekea kuharibika vibaya sura yake.
ajali
Picha ikimwonyesha Norris kabla hajapata ajali, alivyopata ajali na baada ya kuwekewa uso mwingine wa marehemu
Unaambiwa baada ya ajali hiyo kijana huyo alishindwa kutoka nyumbani kwa takribani miaka 15 na amini usiamini kijana huyo alifanyiwa upasuaji wa kihistoria uliochukua masaa 36 na kupandikizwa uso mpya wa mtu ambaye alishafariki baada ya kupata ajali.
Upasuaji huo ulifanyika katika hospitali ya University of Maryland Medical Center na ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa na sasa kijana huyo anaendelea vyema akiwa mwenye furaha.
sura
Mwonekano wa Norris baada ya Baada ya upasuaji
Kwa kawaida kwa sababu ya maadili ya utabibu watu waliopewa mabaki ya viungo vya wafu hawaruhusiwi kukutana na jamaa au ndugu wa marehemu, lakini Norris hakuweza kujizuia kukutana na Aversano, kutoka Maryland ambaye ni dada wa marehemu.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog