MICHEPUKO SIO DILI..!! AKATWA MAPANGA BAADA YA KUGONGANISHA MABWANA
Bahati Nyamkira amenusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili.
MCHEPUKO usitajwe kwako!
Mrembo aliyejulikana kwa jina la Bahati Nyamkira (20) (pichani), mkazi
wa Kijiji cha Singu, Kata ya Kukirango, Butiama, Mara, amenusurika kifo
baada ya kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili na mwanaume
anayedaiwa kuwa hawara yake kisa kikisemekana ni kumkuta akiwa na hawara
mwingine, (kuwagonganisha).
Tukio hilo la kushangaza lilitokea saa 4 usiku wa Mei 23, mwaka huu nyumbani kwa mwanamke huyo katika kijiji hicho.
Kwa mujibu wa mashuhuda,
siku ya tukio, saa 2 usiku, kijana mmoja aitwaye Nyamkinda James (23),
mkazi wa Kijiji cha Buturu ambaye anadaiwa aliwahi kuishi na mwanamke
huyo na kuzaa naye mtoto mmoja, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo kwa
lengo la kumchukua ili aende kulala naye kwao lakini mwanamke aligoma
na kumfanya mwanaume huyo kutia shaka kwamba, huenda ana mwanaume
mwingine.
Ilizidi kudaiwa kuwa,
mara baada ya mwanamke huyo kugoma, kijana huyo aliondoka kimyakimya
hadi nyumbani kwao na kuchukua panga kisha akarudi kwa kunyatia na
kujificha sehemu.“Yule kijana akiwa amejificha huku macho yakiwa kwenye
nyumba ya mwanamke huyo, ghafla alimwona mwanaume mwingine akifika
nyumbani hapo na kugonga mlango.
“Mwanamke alifungua
mlango na kuondoka na mwanaume huyo. Ndipo Nyamkinda alitoka pale
alipokuwa amebana na panga lake na kumvamia kisha kuanza kumcharanga
hovyo mwanamke huyo na kumsababishia majeraha makubwa,” alisema shuhuda
mmoja.
“Sisi tulisikia kelele
kutoka nyumbani kwa Bahati, tulipofika tulimkuta anagaragara chini huku
akitokwa na damu nyingi mwilini na akilia kwa uchungu.“Tulipomuuliza
kulikoni alisema amecharangwa mapanga na hawara yake wa zamani baada
ya kumwona akiondoka na mwanaume mwingine, hivyo tukampa msaada wa
kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Butiama ambako amelazwa,” aliongeza
shuhuda huyo.
Afisa mmoja wa polisi
mjini Butiama ambaye ameomba jina lake lisitajwe kwa kuwa siyo msemaji,
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, mtuhumiwa huyo anasakwa
baada ya kutokomea kusikojulikana.
0 comments:
Post a Comment