Home » »

Lowassa atua jijini Mwanza kusaka wadhamini...Mamia Ya Wananchi Wampokea Huku Wakimwita Rais...! Rais!!

MAELFU ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, na wakazi wengine wa jiji la Mwanza, leo Ijumaa Juni 5, 2015, walifurika kwa wingi kwenye ofisi za CCM wilaya ya Nayamagana na ile ya Ilemela, wengine wakitaka kumuona na kupeana mikono na wengine kwa nia ya kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, alipofika jijini Mwanza kutafuta wana CCM wa kumdhamini katika safari yake ya Matumaini. (Kuwania urais wa Tanzania kupitia CCM.)

Madereva texi, waendesha bodaboda, na hata wafanyakazi na wasafiri kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, waliacha shughuli zao kwa muda ili walau wamuone mtangaza nia huyo wa nafasi ya juu kupitia CCM.

Lowassa alichukua fomu, za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania, Alhamisi Juni 4, 2015 pale makao makuu ya CCM, na safari yake ya kusaka wadhamini ilianza “chap chap” pale pale Dodoma, na Mwanza ndio kituo cha kwanza nje ya Dodoma, ambacho Lowassa, ameanza kampeni yake ya kusaka wadhamini.

Picha ni, Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari amechukua fomu za kuomba CCM imteue kuwania urais, Edwrad Lowassa, akipungia mkono maelfu ya wanachama wa chama hicho na wananchi wengine baada ya kupata wadhamini kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Ijumaa Juni 5, 2015. 
Lowassa, akipokea fomu za wadhamini ambazo tayari zimejazwa na wana CCM wilaya ya Ilemele, kutoka kwa Katibu wa CCM wilayani humo, , Loti Olele Mtui Lazaro

Mmoja wa madereva Texi, akionyesha bango la kumuunga mkon o Lowassa, katika safari ya matumaini 2015
Lowassa, akionyesha fomu ambayo tayari imejazwa na wadhamini wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog