Home » »

Polisi Iringa yakamata DVD za Mafunzo ya kigaidi


Jeshi la polisi mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo ya kijeshi yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al shaabab cha nchini Somalia zilizokuwa zikitumika na watoto wa mitaani wanaodaiwa kuwa walikuwa wakichukua mafunzo kwakutumia DVD hizo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari akieleza kuwa mikanda hiyo iliyokuwa ikitumiwa na vijana hao wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16 inaonesha ukatili na mauaji yanayodaiwa kufanywa na kikundi cha kigaidi cha Al shaabab.Mikanda hiyo walikuwa wakiitazama kwa kutumia kompyuta mpakato yaani laptop.

Aidha kamanda Mungi amesema pamoja na mikanda hiyo ya DVD pia jeshi hilo limekamata watu wawili wanaojihusisha na biashara ya bangi wakiwa na magunia matatu ya bangi katika harakati za kufunga bangi hiyo kwenye vifurushi vidogo tayari kuisambaza kwa wateja wao.

Mungi ameongeza kuwa kamata kamata hiyo iliyofanywa na jeshi hilo mkoa wa Iringa pia imekamata nguzo 35 za umeme za shirika la umeme nchini TANESCO, nyaya za kusambaza umeme na vifaa vingine zikiwa zimehifadhiwa kwa watu binafsi wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za kiupelelezi
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog