SIMBA AFUNGUA DIRISHA LA GARI NA KUUA MTALII AKISHANGAA WANYAMA

Vyombo vikubwa vya
habari vimeripoti sana hii ishu leo June 02 2015, unaweza ukaamua
kufungua kioo ili uone vizuri wanyama wakati uko mbugani unatalii, hii
sio salama sana kwa vile kwenye hifadhi kuna wanyama wengine wakali kama
simba ambao wanaweza kufanya chochote kibaya wakipata nafasi.
Niliwahi kukuwekea
kipande cha video kilichoonesha simba wakifungua mlango wa gari ya watu
waliokuwa wakitalii mbugani, lakini simba hakuwadhuru.. Hii nyingine
imetokea South Africa, kwenye hifadhi ya wanyama ambayo iko kama umbali
wa Kilometa 30 hivi toka Johannesburg.
Mwanamke alikuwa ndani
ya gari akiendelea kutalii ndani ya Lion Park, akatokea simba jike
mmoja, akavamia kwenye gari kupitia kwenye dirisha la gari na
kumshambulia mwanamke ambaye alifariki kutokana na majeraha makubwa
aliyoyapata.
Askari wa hifadhi
waliwahi na kuwafukuza simba lakini mwanamke alifariki kutokana na
majeraha makubwa aliyoyapata huku mwanaume aliyekuwa akiendesha gari
hiyo akiendelea kupata matibabu baada ya kujeruhiwa pia.. tukio la mtu
kufariki kutokana na kujeruhiwa na simba hii ni mara ya tatu ndani ya
kipindi cha miezi minne ndani ya hifadhi hiyo.
Hii ni video ya simba alivyofungua mlango wa gari.
0 comments:
Post a Comment