Home » »

SOWETO GOSPEL CHOIR WAREKODI VIDEO MAALUMU NA CHAKACHAKA KWA AJILI YA MANDELA


Yvonne Chakachaka katika pozi.

Kundi la Soweto Gospel Choir (S.G.C) jumatatu iliyopita lilikuwa studio pamoja na kundi la Black Mambazo wakirekodi video ya wimbo ''A Magnificent Man'' walioshirikishwa na mwanamama Yvonne Chakachaka ukiwa maalumu kwa ajili ya heshima ya Rais wa kwanza wa nchini kwao Nelson Mandela ambaye mwezi huu atakuwa akitimiza miaka 94 tangu kuzaliwa kwake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kundi la Soweto Gospel Choir ambalo pia ni balozi katika mfuko wa Rais huyo mstaafu wamesema, wimbo huo utaonyeshwa tarehe 18 mwezi huu umoja wa mataifa(UN) ikiwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mzee Madiba. Waimbaji binafsi na makundi mbalimbali nchini Afrika ya kusini yamekuwa katika matayarisho mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa rais wao huyo wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia tangu ulipoisha utawala wa makaburu nchini humo.



Kundi zima la Soweto Gospel Choir katika picha ya pamoja.

Baadhi ya waimbaji wa S.G.C nyuma ya jukwaa.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog