ASHA ROSE MIGIRO AREJEA NYUMBANI.
Mratibu
Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (katikati) akiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro aliyemaliza
muda wake leo wakati akirejea nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.
Baadhi ya
Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja
na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wakiwa wamejipanga kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.
Msafara
wa Dr. Asha Rose Migiro ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
Mh. Benard Membe (gari la pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.
Dr. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga Ardhi ya Tanzania.
Dr.
Asha Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na zawadi za maua kutoka kwa
ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje
waliofika kumlaki.
Dr.
Asha Rose Migiro akisalimiana na baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa
na Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr.
Asha Rose Migiro akiendelea kusalimiana na Baadhi ya Mabalozi. Kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe
sambamba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic
Kacou.
Dr.
Asha Rose Migiro (katikati), akizungumza na waandishi wa habari nchini
Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa ambapo pamoja na mambo Mengi amesisitiza kwamba
hatojihusisha na siasa kwa sasa. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe na Kulia ni Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr.
Asha Rose Migiro akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius
Nyerere. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mh. Bernard Membe.
Dr.
Asha Rose Migiro (katikati) akiteta jambo Waziri Membe sambamba na
Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa
na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto)
waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Mwl. J.K Nyerere.
Mbunge
wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akimpongeza Dr. Asha Rose Migiro
kwa kazi nzuri alipokuwa akitumikia kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa walipokutana leo katika Uwanja wa ndege.
Pichani
Juu na Chini ni wakinamama wakimwimbia Happy Birthday Dr. Asha Rose
Migiro ikiwa ni maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa aliporejea nyumbani
leo.
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani kwa Dr. Migiro (hayupo pichani)
Dr.
Asha Rose Migiro akizungumza Jambo na Dr. Alberic Kacou wakati
wakitizama burudani ya ngoma iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake.
Kushoto ni Waziri Membe.
Dr. Migiro akiwasalimia wasanii wa kikundi cha ngoma.
"Karibu tena Nyumba Mama"... Waziri Membe akiagana na Dr. Asha Rose Migiro baada ya mapokezi.
Dr. Asha Rose Migiro akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiondoka katika uwanja wa ndege w
0 comments:
Post a Comment