Home » » KWA TAARIFA YAKO--FAHAMU ALBUM YA ''YESU NI BWANA'' YA MZEE COSMAS CHIDUMULE MAMBO YALIVYOKUWA

KWA TAARIFA YAKO--FAHAMU ALBUM YA ''YESU NI BWANA'' YA MZEE COSMAS CHIDUMULE MAMBO YALIVYOKUWA

cosmas wakati akiimba moja kati yua nyimbo zake
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina ukweli utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Hii leo KWA TAARIFA YAKO ni kwamba mwimbaji nguli wa siku nyingi nchini mzee Cosmas Chidumule ambaye alianza kutamba katika medani ya muziki wa injili nchini mwaka 1999 baada ya kutoa album yake ya kwanza ya injili iitwayo ''YESU NI BWANA''. Nikwamba kwa taarifa iliyonayo GK mzee Chidumule baada ya kuokoka aliamua kutulia nyumbani na kuhudhuria ibada kanisani pekee.


Siku moja kwaya ya vijana Msasani Lutheran wakati huo wakitamba na wimbo wao wa ''Nakushukuru Mungu umenitoa mbali''(kwasasa wanafahamika kama Ukombozi Choir) walikuwa na sherehe fulani hivyo miongoni mwao wakapendekeza kumwalika mzee huyo ambaye alifika na kuimba pambio kama tatu kama sio nne, baada ya hapo aliipenda sana safu ya muziki ya kwaya hiyo ikiongozwa na mpiga solo maridadi Norman.


Kutokana na kazi njema aliyoifanya kwenye sherehe hiyo, kwaya hiyo ikaamua kumbariki mzee huyo kwa kumlipia gharama za studio pamoja na wapigaji wa kwaya hiyo wakashiriki kikamilifu katika upigaji hadi kufanikisha kutoka kwa album hiyo ya ''YESU NI BWANA'' mazoezi wakifanyia katika kanisa hilo la Kilutheri Msasani.


Ambapo siku album hiyo ilipotoka kila mahali ilikuwa ikipigwa kanda hiyo  '' siku zote tunaimbaa siye Yesu ni Bwana, ukatae ukubali shauri yako Yesu ni Bwana'' ambayo licha ya wimbo huo kuna nyimbo nyingi ambazo ni nzuri katika album hiyo, lakini chaguo kubwa la GK ilikuwa wimbo uitwao ''Libarikiwe neno hili la uzima wa rohoni''.


Baada ya kutoka kwa album hiyo ndipo safari kamili ya kuimba muziki wa gospel ikaanza kwa kasi kupitia mwinjilisti Cosmas Chidumule ambaye kwasasa ana album zaidi ya mbili. Mara ya mwisho GK kukutana na mwimbaji huyu ni takribani miaka 4 iliyopita akiwa ni muumini wa kanisa la Kinondoni Revival T.A.G. 

 
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog