Home » »

MWANDISHI WAPO RADIO KUAGWA LEO KIJICHI

Mwili wa mtangazaji na muandaaji msaidizi wa Michezo wa WAPO Radio FM, Joseph Pancras Mapunda utaagwa leo nyumbani kwake Mtoni Kijichi - Bujonga kuanzia saa nane mchana, baada ya kufanyika ibada. Ratiba nzima ya shughuli iko kama ifuatavyo.

Saa 5 - 6:00 Mchana   -   Chakula Nyumbani kwa Marehemu
Saa 6 - 7:00 Mchana   -   Mwili wa marehemu kuwasili nyumbani
Saa 7 - 8:00 Mchana   -   Ibada - nyumbani kwa marehemu
Saa 8 - 9:00 Mchana   -   Kuaga mwili wa marehemu
Saa 9 -10:00 Alasiri -  Safari ya kwenda kuupumzisha mwili (makaburi ya Chang'ombe maduka mawili)
Saa 10 Jioni                -   Ibada - (makaburi ya Chang'ombe maduka mawili) Hapa ndipo itakuwa mwisho wa safari ya mpendwa wetu Joseph Mapunda.

Jinsi ya kufika nyumbani kwa marehemu, panda magari ya Mtoni Kijichi au Mbagala Kuu, shuka kituo cha mwisho (CCM) hapo utatembea kama mita mia moja, kuna kituo kinaitwa Zahanati, hapo kuina transfoma kubwa, utakata kona mkono wa kulia, na hapo utakuwa umefika maeneo ya msibani. (kwa Bujonga)
Joseph Mapunda, pia amekuwa kocha wa timu ya WAPO FC kipindi cha uhai wake.
Kwa wale wanaopenda kushiriki rambirambi, wanaweza kufika WAPO Radio FM na kuonana na Joyce Matthew, ama kwa walio mbali, wanaweza kushiriki kwa kutuma mchango wao kupitia tiGO Pesa na M-Pesa kwa namba 0717-572-066 na 0767-572-066.
Joseph Pancras Mapunda, ama kwa jina la utani 'BABU' kama ambavyo amekuwa akiitwa na wanamichezo wenzake WAPO Radio FM, amefariki siku ya jumamosi katika hospitali ya wilaya ya Temeke alipokuwa amelazwa kuanzia alhamisi usiku. kesho yake ijumaa - alikuwa kwenye matibabu, lakini ilipofika jumamosi, ambapo wafanyakazi wenzake walikwenda kumjulia hali baada yakuwa na kikao, ndipo wakakuta mapazia ya kijani yamezungushiwa kwenye kitanda cha Joseph. Madaktari wanasema, Joseph alikuwa na uvimbe tumboni, ndio uliopelekea kumchukua.
Mshtuko ulikuwa mkubwa, uliojawa na hofu - Joseph Mapunda alikwishatangulia, na kuacha mjane na watoto wawili, ambao bao ni wanafunzi shule ya msingi.
Bwana ametoa, na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog